HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 20, 2016

DKT. SHEIN APIGA KURA UCHAGUZI WA MARUDIO ZANZIBAR LEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika foleni ya wapiga kura ya Uchaguzi wa marudio katika kituo cha kupiga kura Skuli ya msingi Bungi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo,(wa pili kulia) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Dkt.Idriss Muslim Hija.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Ali Mohamed Shein akipokea karatasi ya kupigia kura kutoka kwa PA (1) Jaffar Suleiman kituo namba 1cha kupiga kura ya Uchaguzi wa Marudio Skuli ya Bungi wilaya ya Kati Unguja zoezi ambalo limefanyika leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Ali Mohamed Shein akipiga kura katika uchaguzi wa marudio kituo namba 1cha kupiga kura namba 1 Skuli ya msingi Bungi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo.
Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mama Mwanamwema Shein akiiangalia karatasi ya kupigia kura katika uchaguzi wa Marudio baada ya kukabidhiwa katika chumba namba 3 cha Skuli ya Msingi Bungi Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Viongozi mbali mbali waliomsindikiza wakati alipokwenda kupiga katikauchaguzi wa marudio leo katika kituo namba 1cha Skuli ya Msingi Bungi Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae ni mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk.Ali Mohamed Shein akifanya mahojiano na waandishi wa habari na kuwaonesha kidole kilichoingizwa wino maalum baada ya kipiga kura ya marudio leo katika kituo namba 1 cha Skuli ya Msingi Bungi Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja.Picha na Ikulu, Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad