JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI
“PRESS RELEASE” TAREHE 02.02.2016.
· WAZEE WAWILI WAMEUAWA KIKATILI WILAYANI KYELA MKOANI MBEYA KUTOKANA NA IMANI ZA KISHIRIKINA.
· MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MAPAMBANO JIJINI MBEYA AFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI.
· MWENDESHA PIKIPIKI AFARIKI DUNIA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA GARI KUGONGANA NA PIKIPIKI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
WAZEE WAWILI WAKAZI WA KITONGOJI CHA BULINDA WILAYA YA KYELA MKOANI MBEYA WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. GENELI KAPWELA [65] NA 2. RAHABU BUNGULU [70] WALIUAWA KWA KUKATWA NA VITU VYENYE NCHA KALI SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI YAO NA KISHA KUCHOMWA MOTO NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI.
MIILI YA MAREHEMU ILIKUTWA KATIKA NYUMBA WALIMOKUWA WAKIISHI MNAMO TAREHE 01.01.2016 MAJIRA YA SAA 08:00 ASUBUHI HUKO KITONGOJI CHA BULINDA, KIJIJI/KATA YA MATEMA, TARAFA YA NTEMBELA WILAYA YA KYELA MKOA WA MBEYA.
KATIKA TUKIO HILO, GENELI KAPWELA ALIUAWA KWA KUTENGANISHWA KICHWA NA KIWILIWILI NA KUKATWA MKONO WA KUSHOTO NA VIUNGO HIVYO HADI SASA HAVIJULIKANI VILIPO NA RAHABU BUNGULU ALIUAWA KWA KUCHOMA NA KITU CHENYE NCHA KALI NA WANANCHI WALIOAMUA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI.
INADAIWA KUWA, WANANCHI HAO WALIVAMIA NYUMBA WALIYOKUWA WAKIISHI MAREHEMU KISHA KUWAKATA NA VITU VYENYE NCHA KALI NA BAADA YA KUTEKELEZA MAUAJI HAYO, WATU HAO WALIANGUSHA NYUMBA WALIYOKUWA WAKIISHA AMBAYO ILIKUWA IMEJENGWA KWA MIANZI NA KISHA KUICHOMA MOTO.
CHANZO CHA TUKIO HILO NI IMANI ZA KISHIRIKINA KWANI MAREHEMU WALIKUWA WANATUHUMIWA KULETA UGONJWA WA KIPINDUPINDU KIJIJI HAPO KWA NJIA ZA KISHIRIKINA. WATU WAWILI WAMEKAMATWA KWA MAHOJIANO KUHUSIANA NA TUKIO HILO AMBAO NI 1. ALIKO MWAMTOBE [47] MKAZI WA MATEMA NA 2. ALISOLOMON MWAMTOBE [49] MKAZI WA KITONGOJI CHA BULINDA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUACHA IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA MADHARA MAKUBWA KATIKA JAMII.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MWANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI MAPAMBANO ILIYOPO JIJINI MBEYA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FELISTA MWANSASU [12] AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T.949 CVS AINA YA MITSUBISHI FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA NSAJIGWA ALISALA [39] MKAZI WA MBEYA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 01.01.2016 MAJIRA YA SAA 07:50 ASUBUHI HUKO MAENEO YA MAFIATI, KATA YA MUUNGNANO, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA KATIKA BARABARA YA MBEYA/TUNDUMA.
CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. DEREVA AMEKAMATWA, UPELELEZI UNAENDELEA.
KATIKA TUKIO LA TATU:
MWENDESHA PIKIPIKI ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ASIFIWE MWANTOBE [25] MKAZI WA TUNDUMA MKOANI MBEYA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA PIKIPIKI ALIYOKUWA AKIENDESHA KUGONGANA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 975 CPS AINA YA TATA BUS LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA EMANNUEL ADAM [36] MKAZI WA MBEYA.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 01.01.2016 MAJIRA YA SAA 18:00 JIONI HUKO MAPOROMOKO KATIKA BARABARA YA TUNDUMA/MBEYA, WILAYA MOMBA, MKOA WA MBEYA.
INADAIWA KUWA, MARA BAADA YA AJALI HIYO PIKIPIKI ALIYOKUWA AKIENDESHA MAREHEMU ILITOROSHWA NA WATU WASIOJULIKANA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA TUNDUMA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. DEREVA WA BASI AMEKAMATWA NA UPELELEZI UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO IKIWA NI PAMOJA NA KUFUATA NA KUHESHIMU SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA KUWA MAKINI KATIKA MATUMIZI YA BARABARA HASA KWA KUFUATA SHERIA ZA BARABARANI.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment