HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 9, 2016

Wasichana kunufaika na kampeni maalumu ya Afya.

-Kupitia ujumbe wa simu za mkononi
WASICHANA Nchini kuanzia leo wataanza kunufaika na kampeni maalumu ya kutumia ujumbe mfupi wa maneno kwa njia ya simu za mkononi kwa ajili ya kutoa elimu kwa wasichana kuhusiana na hedhi na jinsi ya kujistiri wanapokuwa kwenye kipindi hicho.

Kampeni hiyo ambayo Taasisi ya Vodacom Foundation kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la T-MARC imewalenga wasichana wenye umri wa kuanzia miaka 18-40  wanaotumia simu za mkononi pia inahamasisha jamii kuacha kuonea aibu mijadala kuhusiana na changamoto za kipindi cha hedhi ambazo zinawakumba wasichana wengi na pia kutoa elimu ni jinsi gani ya kujistiri vizuri ili waendelee na majukumu yao ya kila siku.

Vodacom Foundation imewezesha mradi huu kwa kutoa fursa ya kutuma ujumbe mfupi wa maneno wenye thamani ya shilingi milioni 100 na utatekelezwa na Shirika la T-MARC Tanzania kwa kushirikiana na kampuni ya  PUSH Mobile kwa kipindi cha miezi sita.

Ushirikiano wa Vodacom Foundation na T-MARC unaendelea kutekeleza mradi wa Hakuna Wasichoweza unaondelea katika mikoa ya Lindi a Mtwara ambao kwa kiasi kikubwa meanza kuonyesha mafanikio kwa kupunguza uoro wa wasichana mashuleni wanapokuwa katika vipindi vya hedhi.Mradi huu pia unatarajiwa kuwafikia wasichana  Zaidi ya 10,000 katika mikoa hiyo.

Akiongea kuhusu mradi wakati wa uzinduzi,Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania Ian Ferrao,alisema Vodacom inajivunia kushirikiana na T-MARC kusaidia  afya za wanawake kwa kuwa moja ya dhamira ya kampuni ni kutumia ubunifu wa teknolojia kuboresha maisha ya watu kwenye jamii kama ambavyo imefana kutumia mtandao wake kutoa elimu ya afya na uzazi.

Naye Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO Dk.Moshi Kimizi ambaye alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa  kampeni hii alipongeza Vodacom Foundation na T-MARC kwa kuona umuhimu wa kuelimisha jamii kuhusiana na changamoto za hedhi ambazo zinachangia  wanawake kubaki nyuma.

“Napenda kuungana na kauli mbiu ya kampeni hii,ambayo ni Hedhi sio ikwazo cha kupata elimu kwa wasichana na nawaomba watanzania wote waungane na mimi kuhakikisha kuwa wanashiriki katika kampeni hii kwa kutuma neon MSICHANA kwenda namba 15077 ili kupata taarifa sahihi kuhusiana masuala haya”.Alisema Dk.Kimizi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la T-MARC,Diana Monica Kisaka ameshukuru Vodacom kwa kutoa msaada huu na kudai kuwa utasaidia wasichana wengi kupata elimu ya afya hususani kuhusiana na suala la hedhi na jinsi ya kukabiliana na changamoto zake pia utaweza kupata taarifa Zaidi kuhusiana na ukubwa wa tatizo hili ambalo liko nchini pote.
Takwimu zilizopo juu ya tatizo hili kutokana na utafiti uliofanyika  mwaka 2010 zinabainisha kuwa wasichana wapatao 68,538 wamekatiza masomo yao kutokana na  changamoto za hedhi ambao ni asilimia 75 ya  wanafunzi watoro mashuleni.

Mbali na msaada huu,Vodacom Foundation imeishatumia Zaidi ya shilingi 378 katika mradi wa Hakuna Wasichoweza kati ya mwaka 2014-2015 ambao unaendelea katika mikoa ya Lindi na Mtwara.
 Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Unesco,Dkt Moshi Kimizi(katikati)na Mkurugenzi mtendaji wa T-Marc Tanzania,Diana Kisaka(kushoto) wakimsikiliza Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation,Renatus Rwehimbiza(kulia) wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo(hawapo pichani)katika hafla ya Uzinduzi wa kampeni ya Ujumbe Mfupi(SMS) kwa Njia ya Simu za mkononi kupitia mradi wa”Hakuna wasichoweza”unaotoa elimu bora ya kujisitiri kwa wasichana wakati wa hedhi na Usafi kwa mtoto wa kike ambayo huwafanya wasichana kukosa masomo yao mara kwa mara.
 Mkurugenzi mtendaji wa T-Marc Tanzania,Diana Kisaka(kushoto)na Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation,Renatus Rwehimbiza(kulia) wakimshuhudia Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Unesco,Dkt Moshi Kimizi(katikati)akibofya kitufe cha kompyuta kuashiria Uzinduzi rasmi wa kampeni ya Ujumbe Mfupi(SMS) kwa Njia ya Simu za mkononi kupitia mradi wa”Hakuna wasichoweza”unaotoa elimu bora ya kujisitiri kwa wasichana wakati wa hedhi na Usafi kwa mtoto wa kike ambayo huwafanya wasichana kukosa masomo yao mara kwa mara.Hafla hiyo ilifanyika leo jijini Dar es Salaam. 
 Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Unesco,Dkt Moshi Kimizi(katikati)akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Push Mobile,Freddie Manento(wapili kushoto) wakati wa hafla ya Uzinduzi wa kampeni ya Ujumbe Mfupi(SMS) kwa Njia ya Simu za mkononi kupitia mradi wa”Hakuna wasichoweza”unaotoa elimu bora ya kujisitiri kwa wasichana wakati wa hedhi na Usafi kwa mtoto wa kike ambayo huwafanya wasichana kukosa masomo yao mara kwa mara,Wanaoshuhudia kushoto Mkurugenzi mtendaji wa T-Marc Tanzania,Diana Kisaka na  Mkuu wa kitengo cha Vodacom Foundation,Renatus Rwehimbiza(kulia)
Wafanyakazi wa Wizara ya Elimu, Afya, wafanyakazi wa T-Marc Tanzania na Vodacom wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Uzinduzi wa kampeni ya Ujumbe Mfupi(SMS) kwa Njia ya Simu za mkononi kupitia mradi wa”Hakuna wasichoweza”unaotoa elimu bora ya kujisitiri kwa wasichana wakati wa hedhi na Usafi kwa mtoto wa kike ambayo huwafanya wasichana kukosa masomo yao mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad