Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Lugoba wakiwa Darasani wakijisomea masomo yako wa njia ya Kompyuta.
WANAFUNZI wa shule ya Sekondari ya Lugoba iliyopo Msata-Bagamoyo mkoani Pwani wamefaidika na kompyuta zilizotolewa na kampuni ya simu za mkononi ya Halotel kwaajili ya kusaidia masomo ya TEHAMA shuleni hapo.
Halotel imetoa msaada wa kompyuta 19 pamoja na kuziwekea mtandao wa intaneti yenye spidi kubwa ya kampuni hiyo bure, kwaajili ya kuwezesha wanafunzi wa shule hiyo kujisomea kwa urahisi.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya Lugoba, Abdala Sakasa ameishukuru kampuni ya Halotel kwa kuiangalia shule hiyo kwa jicho la pekee na kuamua kuisaidia kompyuta hizo.
‘Wanafunzi wa dunia ya sasa ni muhimu waweze kutumia mtandao kujifunza na kupata maarifa mbalimbali tofauti na vizazi vilivyopita, na hivyo tunaishukuru Halotel kwa kusaidia kuwezesha hali hii’ alisema mwalimu Sakasa.
Kwa upande wa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Lugoba, wameushukuru mtandao wa Halotel kwa kuwapa msaada wa kompyuta hizo ambazo zimeweza kuongeza ari na juhudi za kujifunza kupitia kompyuta hizo.
‘Tunaishukuru kampuni ya Halotel kwa kutujengea darasa la komputa pamoja na kutupa komputa mpya zilizounganishwa na mtandao wa 3G, hali ambayo imeturahisishia kujifunza kwa vitendo masomo ya TEHAMA’ alisema Asha Mohamed, mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo.
Kampuni ya Halotel yenye kauli mbiu ya Pamoja katika Ubora, inalenga kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma ya mtandao kwa kila sehemu ya Tanzania, ambapo mpaka sasa imeshaunganisha mtandao wa simu kwa zaidi ya vijiji 1500 ambavyo vilikuwa havijaunganishwa na huduma ya mtandao wowote wa simu kutoka mwanzo.
Katika hatua nyingine, kampuni ya Halotel itaweka mkazo wa hali ya juu katika kuboresha mtandao, huduma kwa wateja, huduma kwa jamii hali itakayopelekea mapinduzi katika sekta ya mawasiliano nchini.
Ikiwa na kilomita 18,000 za fibre optic, pamoja na zaidi ya minara 2500, Halotel ndiyo kampuni yenye mtandao mkubwa zaidi nchini, ambayo pia itatumika kuunganisha serikali za mitaa 150, hospitali 150, vituo vya polisi 150, ofisi za posta 65 na intaneti ya bure kwa shule zaidi ya 450.
Hadi sasa Halotel imeshawekeza zaidi ya dola bilioni 1 za kimarekani mpaka sasa kwa kutengeneza miundombinu na kuboresha mtandao wa mawasiliano, kampuni ya Halotel imefanikiwa kufikisha huduma za mtandao katika mikoa yote 26 nchini, pamoja na miji na vijiji, ikiwa ni zaidi ya asilimia 95% ya watanzania wote hivyo kuifanya kuwa kampuni yenye mtandao mkubwa zaidi nchini.
No comments:
Post a Comment