Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiongoza uokoaji wa wananchi walioathirika na mafuriko kijiji cha Pawaga
Na Mwandishi wetu, Iringa
Mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Iringa zimesomba mashamba na nyumba na kuwaacha wananchi wengi wakiwa hawana mahali pa kukaa.
Vitongoji vilivyo athirika sana ni Kisanga, Nyallu, Makoka na Mbughani. Mpaka sasa bado idadi isiyo rasmi inakadiliwa watu zaidi ya 200 bado wamezingirwa na maji siku ya 4.
Juhudi za uokoaji zikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela zimefanikiwa kuokoa watu 399 kitongoji cha Kisinga, watu 38 kutoka kitongoji cha Makoka, na watu 23 kutoka kitongoji cha Nyalu. Jeshi la polisi lilitoa helicopter kusaidia uokoaji na pia kikosi cha Zimamoto na Uokoaji kilikuwa mstari wa mbele kwenye zoezi hilo.
Maeneo mengi yalihitaji waogoleaji mahiri ili kuwafikia wananchi.
Zoezi linaendelea hado sasa. shule 2 zimetengwa kwa ajili ya kupokea wahanga wa mafuriko shule ya msingi Itunundu na shule ya msingi Kisanga.
kitongoji cha Nyalu wamezingirwa na maji
Eneo lililoathirika
Njia haipitiki kwa vyombo vya moto
Familia zikiwa imezingirwa na maji.

Kijiji cha Itunundu ndio kambi kubwa ya uokoaji

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiongwea na na waathirika wakati wa zoezi la uokoaji wa wananchi walioathirika na mafuriko kijiji cha Pawaga

Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Richard Kasesela akiongwea na na waathirika wakati wa zoezi la uokoaji wa wananchi walioathirika na mafuriko kijiji cha Pawaga
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela akikagua athari katika kijiji cha Mapogoro Tarafa ya Idodi Wilayani Iringa
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe Richard Kasesela akiendelea kukagua athari katika kijiji cha Mapogoro Tarafa ya Idodi Wilayani Iringa
No comments:
Post a Comment