Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akifyeka majani kwa ajili ya njia kuelea eneo lilikubwana mafuriko katika eneo la mashamba ya mbunga Nyalu.
Rubani wa ndege ya Jeshi la Polisi, Flora Focas akimwokoa mama mjamzito na kumuingiza katika chopa iliyompeleka Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ambaye aliamuru chopa hiyo imchuke mama huyo ili kuokoa miasha yake.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla akitokea kwenye eneo la pori kwenye mashamba ya mpunga ya Nyalu kwa ajili ya kuangalia watu waliozingirwa na maji ili wawezekuokolewa . Alikuwa amembatana na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mjini, Richard Kasesela.
Akina mama wenye watoto wadogo mtoto wa wiki moja na miezi miwili kuondoka katika eneo la marufiko katika mashamba ya Nyalu lililopo wilaya ya Iringa Mjini.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Kigwangalla akimwangalia mtoto aliyeugua ugonjwa wa kipindupidu
katika kituo cha afya cha Mtakatifu Lucas (Kambi ya ugonjwa huo) kwenye
eneo la Mboliboli kutokana na marufiko yaliyotokea katika kijiji cha
Idodi, Iringa ambayo yalisomba nyumba na vyoo baada ya mto Ruaha kujaa
maji kubadilisha mkondo wake.
Baadhi
ya wagonjwa wakiendelea kunywa maji maalum kwa ajili ya kuongeza nguvu
baada ya kukumbwa na ugonjwa huo katika kambi maalum ya ugonjwa huo
iliyopo katika kituo cha afya cha Mtakatifu Lucas.kwenye wilaya ya
Iringa Mjini.
Baadhi ya maeneo yaliyokumbwa na marufiko katika eneo la mashamba ya mbunga lijulikalo kwa jina la Nyalu.
(Picha na MAGRETH KINABO –MAELEZO)
No comments:
Post a Comment