HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 19, 2016

Maonyesho ya Kibiashara ya Mauritius kuzinduliwa na Waziri wa Viwanda.

Meneja wa kampuni ya Enterprise Mauritius, Rajen Subbamah akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusiana na Maonyesho ya kibiashara ya kimataifa ya Mauritius yanayotarajiwa kuzinduliwa jumatatu na Waziri wa viwanda na biashara, Mh. Charles Mwijage jijini Dar es Salaam yakilenga kujenga mahusiano na kutizama fursa za kibiashara baina ya mataifa haya mawili. Wengine ni Mkurugenzi wa TICC, Bw. David Lutabana (wa pili kulia) na mratibu wa tukio hilo, Bi, Neema Gerald (kulia).
Bw. Paul Koyi, Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Wilaya ya Temeke akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusiana na Maonyesho ya kibiashara ya kimataifa ya Mauritius yanayotarajiwa kuzinduliwa jumatatu na Waziri wa viwanda na biashara, Mh. Charles Mwijage jijini Dar es Salaam yakilenga kujenga mahusiano na kutizama fursa za kibiashara baina ya mataifa haya mawili.
Mkurugenzi wa TICC, Bw. David Lutabana akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam kuhusiana na Maonyesho ya kibiashara ya kimataifa ya Mauritius yanayotarajiwa kuzinduliwa jumatatu na Waziri wa viwanda na biashara, Mh. Charles Mwijage jijini Dar es Salaam yakilenga kujenga mahusiano na kutizama fursa za kibiashara baina ya mataifa haya mawili. Wengine ni Meneja wa kampuni ya Enterprise Mauritius, Rajen Subbamah (wa pili kushoto) na Bw. Paul Koyi, Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Wilaya ya Temeke (kushoto).

Maonyesho ya kibiashara ya kimataifa ya Mauritius yanatarajiwa kuzinduliwa jumatatu na Waziri wa viwanda na biashara, Mh. Charles Mwijage jijini Dar es Salaam yakilenga kujenga mahusiano na kutizama fursa za kibiashara baina ya mataifa haya mawili.

Maonyesho hayo ya siku moja yatafanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere na kushirikisha makampuni zaidi ya 17 kutoka taifa hilo linalotegemea uchumi wa sekta ya uzalishaji.Maonyesho hayo yanaandaliwa na kampuni ya Talemwa Investment (TICC) pamoja na Enterprise Mauritius kwa ushirikiano na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) na Chemba ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana Mkurugenzi wa TICC, Bw. David Lutabana alisema maonyesho hayo ni fursa ya kipekee itakayowakutanisha wafanyabiashara kutoka nchi hizi mbili ili kuweza kubadilishana uzoefu pamoja na kujadili fursa mbalimbali zilizopo katika nchi hizo.

“Wafanyabiashara pamoja na Wazalishaji wetu wa ndani wanaendelea kutafuta fursa za uwekezaji katika masoko mbalimbali na kwa kuzingatia hili, mkutano na maonyesho haya ni fursa adhimu itakayowawezesha kuweza kutanua wigo wao wa kibiashara nchini humo,” alisema.

Aliyataja baadhi ya makampuni yanayoshiriki maonyesho hayo kuwa ni pamoja na Abita Shades, Africasia Electronics Manufacturing, Bacotex Limited, Eurolux, Glory Plastics Ind Ltd, IF Glass, La Trobe Co Ltd, Marble and Stones, Navigation and Geocoding Technologies Ltd, Nivra Enterprises Ltd, Safocean Co Ltd, Sissi Creation, SLK Gold Taste Ltd, SMP International Ltd, Soge International, Top Detergent Ltd na V-Information Technology & Management Institute.

“Natoa wito kwa wafanyabiashara ikiwa ni pamoja na wauzaji wa jumla na wale wanaotaka kuwa mawakala wa bidhaa kutoka Mauritius wajitokeze kwa wingi katika maonyesho haya ili waweze kujionea bidhaa zinazoweza kufaa katika soko la ndani lakini pia kuweza kutengeneza mahusiano na kupata fursa zaidi za kibiashara,” alisema.

Akizungumza wakati wa shughuli hiyo, Meneja wa kampuni ya Enterprise Mauritius, Rajen Subbamah, alisema sekta zitakazoshiriki kutoka Mauritius ni pamoja na sekta ya ukandarasi, bidhaa za kilimo, kemikali, viwanda vya utengenezaji nguo na vidani, pamoja na sekta zingine.

Bw. Subbamah alisema wafanyabiashara hao watatatumia siku ya Jumanne kutembelea wafanyabiashara hapa nchini ili kuweza kutambua mahitaji yao lakini pia kuweza kujifunza ni jinsi gani wanavyoendesha shughuli zao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad