HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 24, 2016

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU MGENI RASMI KATIKA TAMASHA LA PAMOJA TUNAFANIKISHA.

Na M wandishi wetu.
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan (Pichani) mgeni rasmi Tamasha la Pamoja Tunafanikisha litakaloandaliwa na kampuni ya Trumark katika kusherehekea maadhimisho ya siku ya mwanamke Dunia.

Akizungumza na mwandishi wetu kwa njia ya simu, Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark Agnes Mgongo ambaye ndie mwenyekiti wa maandalizi ya tamasha hilo amesema mama Samia pamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya wanawake watakutana siku ya Machi tano ili kusheherekea mafanikio ya mwanamke pamoja na kuziangalia changamoto zinazomzunguka na kuzibadili kuwa fursa.

“Kwa kweli tamasha hili litakuwa la aina yake ikizingatiwa hii ni mara ya kwanza kwa nchi yetu kuwa na makamu wa Rais mwanamke tangu kupatikana kwa uhuru, hii itatoa fursa kwa wanawake kuamini kuwa tunaweza kutimiza ndoto zetu kwenye safari ya mafanikio”alisema Agnes.

Agnes amesema Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inalenga katika kuwaleta pamoja wanawake na wanaume na kutoa ahadi zao za kuwa mabalozi wa kuharakisha harakati za usawa wa kijinsia katika maeneo yanayowazunguka.

Ameongeza kuwa tamasha hilo litakuwa jukwaa la kukutanisha wanawake kutoka fani na kada tofauti ili kutengeneza mtandao ambao utakuwa chachu muhimu kwa ustawi wao ambapo tamasha hilo litaenda sambamba na watoa mada kutoka nyanja mbalimbali kama vile uchumi na fedha, ujasiliamali na masuala ya afya maonyesho ya biashara ya bidhaa za ubinifu kutoka kwa wanawake, chakula cha usiku na burudani ya muziki kutoka kwa wasanii wa hapa nchini akiwemo Elias Barnaba na bendi yake ya Clasicc ,mkogwe wa muziki wa taarab Mama Patricia Hillary na Misoji Mikwabi ambao wataongozwa na mchekeshanji maarufu MC Pilipili.

Agnes aliwashkuru wadau mbalimbali wakiwemo King Solomon Hall, Valleys Spring, Mummys Exclusive Shop, Flexible Entertainment, Channel Ten na Magic Fm. Pia aliwakaribisha wadau wote kuungana pamoja katika siku hii muhimu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad