HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 10, 2016

KAMPUNI YA TRUMARK HAPA NCHINI KUANDAA MAADHIMISHO YA PAMOJA TUNAFANIKISHA KUSHEREKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI MACHI 5 MWAKA HUU.


Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kampuni ya Trumark hapa nchini, Agnes Mgongo akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya wanawake Duniani ambayo hufanyika Machi 8 kila mwaka ambapo mwaka huu kitaifa itafanyika mkoni Mbeya na kwa kampuni ya Trumark kuazimisha Machi 5, katika ukumbi wa King Solomoni Uliopo eneo la Namanga jijini Dar es Salaam.Tamasha hilo likiwa na lengo la kuungana na wanawake wote duniani kusherekea mafanikio ya mwanamke na kuangalia changamoto zinazomzunguka na kugeuza kuwa Fursa.


Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kampuni ya Trumark hapa nchini, Agnes Mgongo (kulia) akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Mratibu wa Tamasha la siku ya wanawake duniani wa kampuni ya Tremark, Daria Erasto.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Trumark hapa nchini wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kampuni ya Trumark hapa nchini, Agnes Mgongo (aliyekaa) na waliosimama ni waratibu wa Tamasha la kuadhimisha siku ya wanawake litakalofanyika Machi 5 katika ukumbi wa King Solomon uliopo upanga (Kutoka kulia) ni Pulcheria Mendera, Azavery Phares(katikati) na Daria Erasto.

Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.


KAMPUNI ya Trumark hapa nchini kuandaa maadhimisho ya pamoja tunafanikisha kusherekea siku ya wanawake Duniani machi 5 katika ukumbi wa King Solomon ulipo maeneo ya Namanga jijini Dar es Salaam.


Maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani hufanyika Machi 8 kila mwaka kila mwaka ambapo mwaka huu kitaifa yatafanyika Mkoani Mbeya yakiwa na lengo la kuungana na wanawake wengine woe duniani kusherekea mafanikio ya mwanamke na kuangalia changamoto zinazomzunguka na kuzigeuza kuwa fursa.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kampuni ya Trumark hapa nchini, Agnes Mgongo wakati akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam leo, amesema kuwa wa kampuni ya Trumark inajihisisha na utoaji mafunzo na uwezeshaji kwa wanawake na vijana, wakati wa kuelekea kilele cha maazimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, pia kampuni hiyo imekua ikiadhimisha siku ya wanawake kwa takribani miaka mitano sasa na kumekuwa na mafanikio makubwa kwani wahudhuriaji wengi wamekuwa na mrejesho chanya, nakuongeza mtandao katika shuguli zao mbalimbali.

Agnes ameiasa Jamii ya kitanzania kuungana pamoja kushirikiana ili kuleta usawa wa kijinsia, kufikia mwaka 2030 kuwe na uwakilishi wa asilimia 50 kwa 50 katika nyanja zote, kisiasa, kiuchumi na kijamii baina ya wanawake na wanaume, baada ya umoja wa mataifa kuja na malengo endelevu 17.

“ Mwaka huu ni wa kwanza baada ya umoja wa Mtaifa(UN)kuja na malengo mapya 17 ya maendeleo endelevu(SDG’S) baada ya kuisha muda mrefu kwa malengo nane ya mi

lenia yaliyowekwa na umoja huo mwaka 1990,ikiwa Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani, wanawake wenyewe wana fursa kubwa ya kujitathimi na kujitambua wanahitaji nini katika maisha yao” amesema Agnes.

Amesema kuwa Trumark imepata Baraka zote kutoka wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika kuandaa siku hii muhimu, kwenye maadhimisho haya kutakuwa na mada ambazo zitatolewa kutoka kada tofauti juu ya uongozi, biashara, uchumi na ujasiriamali, pia katika tamasha hili pia kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbli wa hapa nchini na chakula cha usiku katika kusheherekea mafanikio ya wanawake.

Aidha Agnes amesema kuwa watakaohudhulia watapata fursa ya kupimwa bure kwa hiari na kuhamasishwa kufanya mazoezi na kuwaelezea faida ya mazoezi ili kujenga afya bora na kuepukana magonjwa yale yasiyo yakumbukizwa lakini hatari kama kisukari, shinikizo la damu na uzito uliozidi (obesity).

Pia amesema kuwa kutakuwa na fursa kwa wafanyabiashara wanawake kujitangaza kwa kufanya maonyesho ya bidhaaa zao mbalimbali ili kujitangaza na kujiongezea wateja.

Agnes amewakaribisha wahisani na wadau mbalimbali wanaojihusisha na maswala mbalimbali ya Wanawake kujitokeza na kushiriki pamoja katika siku hii muhimu kwa jamii yetu.Kwa mawasiliano 
Daria Erasto 
Afisa Uhusiano 
Trumark 
+255 716 676665/ 754 095017 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad