HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 16, 2016

TAARIFA YA KUZIMWA KWA MTAMBO WA MAJI WA RUVU JUU

Shirika la Maji Safi na Majitaka Dar-es-salaam (DAWASCO), Linasikitika kuwatangazia  wakazi wa jiji la Dar-es-salaam na  Mji wa Kibaha mkoan pwani kuwa Mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Juu utazimwa kwa wastani wa Saa 36 kwa siku za Jumatatu 18/01/2016 na Jumanne 19/01/2016.

Mtambo wa Ruvu Juu utazimwa ili kuruhusu Mkandarasi Kumalizia kazi za Ujenzi kwa kuunganisha Pampu za Mtambo mpya Mtoni. Zoezi hili linaashiria kukamilika kwa upanuzi wa Mtambo wa Maji wa Ruvu juu. Shirika linakusudia kuzalisha maji mapya toka Mtambo wa Ruvu Juu kuanzia tarehe 28 Februali 2016 na Kuondoa kabisa tatizo la maji kwa maeneo yanayohudumiwa na Mtambo wa Ruvu Juu

Kuzimwa Kwa mtambo wa Ruvu Juu kutapelekea maeneo yafuatayo katika Jiji kukosa Maji:

MLANDIZI, KIBAHA, KIBAMBA, MBEZI, KIMARA, UBUNGO, KIBANGU, MAKUBURI PAMOJA NA ENEO LOTE LA TABATA.

WANANCHI MNASHAURIWA KUHIFADHI MAJI NA KUYATUMIA KWA MATUMIZI YA LAZIMA.

Wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 022-2194800 au 0800110064 (BURE)
DAWASCO INAWAOMBA RADHI WANANCHI KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA.

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad