Mwandishi wa Habari Mwandamizi wa Michuzi Blog, Chalila (kushoto) akikabidhiwa na Kaimu Mkuu wa Habari Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Clarence Nanyaro cheti maalumu cha kutambua mchango wa blogu hiyo namna ilivyoshiriki katika kurusha matangazo, mijadala, habari na michezo iliyoelimisha na kuhamasisha wananchi kujitokeza katika shughuli mbalimbali za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Hafla hiyo ya kukabidhi vyeti kwa vyombo vya habari vilivyofanya vizuri kazi hiyo, ilifanyika Makao Makuu ya NEC Dar es Salaam leo.
Thursday, January 28, 2016
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment