Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts, Juma Pinto (kushoto),
akimuelezea Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Richard Mwaikenda
kuwa wakati gazeti la Jambo Leo lilipoanzishwa 2009, alikuwa mfanyakazi
wa kwanza kujiunga na gazeti hilo akitokea Kampuni ya Business Times.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts, Juma Pinto (kushoto),
akimuelezea Mhariri wa Habari wa Gazeti la Jambo Leo, Said Mwishehe kuwa
wakati gazeti la Jambo Leo lilipoanzishwa 2009, alikuwa miongoni mwa
wafanyakazi wa kwanza kujiunga na gazeti hilo akitokea Kampuni ya
Business Times.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Jambo Concepts, Juma Pinto (kushoto),
akimuelezea Mwandishi Mwandamizi wa Michezo na Burudani, Asha Kigundula
kuwa wakati gazeti la Jambo Leo lilipoanzishwa 2009, alikuwa miongoni
mwa wafanyakazi wa mwanzo kujiunga na gazeti hilo akitokea Kampuni ya
Business Times.
Mpigapicha
Mkuu wa Jambo Leo na magazeti mengine ya Staa Spoti na Jambo Brand
Tanzania, Richard Mwaikenda, akitoa shukrani wakati wa hafla hiyo
Baadhi ya wafanyakazi wa Gazeti la Jambo Leo na familia zao, wakigongeana glasi zenye vinywaji ikiwa ni ishara ya kutakiana heri wakati wa hafla ya kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha ya Mwaka Mpya 2016, katika Mgahawa wa City Sports Lounge, Dar es Salaam
Wafanyakazi wa Jambo Leo na familia zao pamoja na wageni waalikwa wakiburudika kwa muziki uliokuwa ukiporomoshwa wakati wa hafla hiyo iliyofanyika kwenye Mgahawa wa kisasa wa City Sports Lounge, katikati ya Jiji la Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA
Mhariri wa Michezo na Burudani wa Gazeti la Staa Spoti ambalo ni gazeti dada la Jambo Leo, Zahoro Mlanzi akigawa 'champagne' kwa wafanyakazi wenzake wakati wa hafla hiyo.
Mpiga Picha Mkuu wa Gazeti la Jambo Leo, Richard Mwaikenda (wa pili kulia), akijadiliana jambo na wakurugenzi wa Kampuni za Jambo Concerpts Tanzania Limited na Jambo Communication, Theophil Makunga (kushoto), Benny Kisaka (wa pili kushoto) na Juma Pinto wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa gazeti la Jambo Leo, wakiwa na furaha wakati wa hafla hiyo ya kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha Mwaka Mpya 2016, Dar es Salaam juzi. Kutoka Kushoto ni Stellah Kessy, Magendela Hamis, Salha Mohamed, Celina Mathew, Suleiman Msuya na Edith Msuya.
Wakipata mlo wa usiku
Mfanyakazi Moi Dodo akiwa na wife wake
Champagne zikifunguliwa
Asha Kigundula akiwamiminia champagne wanahafla
Mwishehe na Kigundula wakikumbatiana kwa furaha
Sasa ni wakati wa kusakata muziki
Ni furaha tele
No comments:
Post a Comment