Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akizungumza na raia wa China
wanaoishi nchini, katika sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika
katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba
yake, Waziri Kitwanga alisema Tanzania inatambua ushirikiano mzuri wa miaka
mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate
taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa
kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali.
Kaimu
Balozi wa China nchini, Zhang Biao akizungumza katika sherehe ya raia wa China
wanaoishi nchini ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa
Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam, kabla ya kumkaribisha Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (hayupo pichani) kuja kuzungumza na
mamia ya wachina hao waliohudhuria sherehe hiyo. Katika hotuba yake, Waziri
Kitwanga alisema Tanzania inatambua ushirikiano mzuri, wa miaka mingi uliopo
kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za
kuishi Tanzania, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni
nchini, kamwe haitagusa wenye vibali halali.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto), kwa kutoa hotuba nzuri iliyowafafanulia
wachina waishio nchini kuwa Serikali ya Tanzania inawajali na inatambua umuhimu
wa ushirikiano wao uliodumu kwa kipindi cha miaka mingi, hivyo raia yeyote wa
kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi Tanzania, na operesheni inayoendelea
ya kuwakamata raia wa kigeni nchini, kamwe haitagusa wenye vibali halali.
Wachina waishio nchini jana walifanya sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika
katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip na kuhudhuriwa na mamia ya wachina hao.
Kulia ni Kaimu Balozi wa China nchini,
Zhang Biao
Raia
wa China wanaoishi nchini wakishindana kula Tunda aina ya Tikiti wakati wa
Sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya
Golden Tulip, jijini Dar es Salaam. Katika Sherehe hiyo ambayo Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (hayupo pichani) alikuwa mgeni rasmi
ilihudhuria na mamia ya raia hao wa China. Hata hivyo, Waziri Kitwanga alisema raia
yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi Tanzania, na operesheni
inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni nchini, kamwe haitagusa wenye vibali
halali.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akiwapongeza raia wa China walioshinda
mchezo wa bahati nasibu walioucheza katika sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya
iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam.
Waziri Kitwanga katika hotuba yake alisema nchi yake inatambua ushirikiano
mzuri wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni
anatakiwa afuate taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea ya
kuwakamata raia wa kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali.
Kikundi cha Karate
kinachoongozwa na raia wa China wanaoishi nchini kikitoa burudani katika
sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya
Golden Tulip, jijini Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles
Kitwanga (hayupo pichani) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hiyo,
katika hotuba yake alisema nchi yake inatambua ushirikiano mzuri wa miaka mingi
uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate
taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa
kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali.
Sehemu ya raia wa China
wanaoishi nchini, wakimsikiliza kwa makini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba yake kwa
Wachina hao katika sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika
Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam jana. Waziri Kitwanga
katika hotuba yake alisema nchi yake inatambua ushirikiano mzuri wa miaka mingi
uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate
taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa
kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali. Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment