HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 21, 2016

Jeshi la Zimamoto latoaji elimu ya majanga ya moto kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Temeke

Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji FC Chenjelai John akimuelekeza Mwanafunzi Enea Gerald wa shule ya Sekondari Temeke jinsi ya kukabiliana na moto ukiwa katika hatua ya awali tarehe 20 Januari 2016. Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeamua kuwekeza katika utoaji wa elimu ya majanga ya moto kwa watoto wadogo na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ili kutengeneza jamii yenye ufahamu na utayari wa kukabiliana na majanga ifikapo mwaka 2025.
Kijue kifaa kinacho weza kung’amua moshi kutoa taarifa; Kinaitwa smock detector kinauwezo wa kung’amua moto kwa kupitia moshi kasha kupiga alam. Kifaa hiki kina patikana katika maduka yanayouza vifaa vya kuzimia moto na bei yake ni ya kawaida sana. Hakizimi moto kazi yake ni kutoa taarifa ili wewe mwananchi ujue mapema kabla moto hauja samba na kuleta madhara makubwa.
Ili kifaa hiki kikusaidie lazima uwe na mtungi wa kuzimia moto wa huduma ya kwanza sambamba na kutoa taarifa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kupiga namba ya dharura 114.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad