Timu ya kuogelea ya Isamilo kutoka mkoa wa Mwanza na Dar Swim Club zimetamba kutwaa nafasi ya kwanza katika mashindano ya kuogelea ya Tallis yaliyopangwa kuanza Ijumaa Januari 29 na kumalizika Jumamosi Januari 30 kwenye bwawa la kuogelea la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika ( IST Upanga).
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Mwanza jana, Mwenyekiti wa Klabu ya Kuogelea ya Mwanza (MSC), Jason Miller alisema kuwa wamejiandaa vilivyo kutwaa medali za dhahabu katika mashindano hayo amayo yatafanyika kwa siku mbili.
Miller alisema kuwa klabu ya Isamilo ndiyo inawakilisha mkoa huo katika mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kushirikisha waogeleaji zaidi ya 400 kutoka klabu mbalimbali hapa nchini.

Peter
Itatiro wa Dar Swim Club akionyesha umahiri wake katika kuogelea. Peter
ana miaka 9 atashiriki katika aina nne ya mashindano hayo kwa staili
zote.
Alisema kuwa wamecagua waogeleaji 21 kwa ajili ya mashindano hayo na kwa muda wote walikuwa katika mazoezi makali. “Najua kuna ushindani mkubwa sana katika mashindano , tulifanya mazoezi kwa muda mrefu na kuwashindanisha staili mbalimbali za kuogelea kwa kuzingatia muda, wote wameonyesha muda mzuri na tupo tayari kwa mashindano,” alisema Miller.
Aliwataja wachezaji wake kwa upande wa wasichana kuwa ni Anna Guild, Emma Imhoff, Bridget Peck, Rebecca Guild, Nandi O’Sullivan, Natalie Mulford, Sachi Buggana, Sofia Sanchez, Isobel Sanchez, Umi Kulthum na Maisah Pirani.
Kwa upande wa wavulana ni Matthew Guild, Elia Imhoff, Eric Nixon, Khaleed Razac, Judah Miller, Caleb O’Sullivan, Delvin Barick, Jack Peck, Daniele Imhoff na Ezra Miller.
Wakati Isamilo ikitamba, klabu maarufu ya Dar Swim Club nayo imetamba kulibakisha taji la mashindano hayo kutokana na mazoezi ambayo wameyafanya.
Katibu Mkuu wa Dar Swim Club, Inviolata Itatiro alisema jana kuwa wamejiandaa vilivyo kwa ajili ya kutwaa medali nyingi za zawadi na hasa ukizingatia kuwa waogeleaji wao wana uzoefu wa kimataifa.
Inviolata alisema kuwa hivi karibuni walifanya vyema katika mashindano yaliyofanyika nchini Dubai na kushirikisha waogeleaji kutoka nchi mbalimbali duniani huku wao wakiwa wanashiriki kwa mara ya kwanza.

“Tulishinda medali za dhahabu katika mashindano hayo, waogeleaji wetu wamepata uzoefu mkubwa, naamini watafanya vyema,” alisema Inviolata ambapo jumla ya waogeleaji 50 wataiwakilisha klab hiyo.
Waogeleaji hao ni Meyia Avery, Anna Azzoni, Chinwe Bruns, Joshua Bruns, Isobel Bush, Klaryce Durand, Smriti Gokan, Bailey Golembeski, Carter Golembeski, Celina Itatiro, Lidia Janik, Ursulla Khimji, Mayli Kiepe, Naaliyah Kweka, Saffiro Kweka, Lois Scheren, Diya Shah, Maya Somaiya, Niki Somaiya, Kelya Temba, Maia Tumiotto, Lara Van Den Hombergh na Chichi Zengeni ambao ni wasichana.

Waogeleaji wa klabu ya Dar Swim Club walifanya mazoezi kwa ajili ya
mashindano ya Tallis yaliyopangwa kuanza Ijumaa kwenye bwawa la kuogelea
la Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) Upanga.
Kwa upande wa wavulana ni Timothee Callens, Sebastian Carpintero, Raahi Davda, Jean De Villard, Marin De Villard, Victoire De Villard, Flore De Villeneuve, Gaspard De Villeneuve, Luwe De Wet, Joaquim Deering, Lisa Di Stefano,Josh Golembeski,Matt Golembeski, Peter Itatiro, Jonathan, Lubuva, Adrien Madjitoloum, Reuben Monyo, Emmanuele Moroni, Rodolfo Moroni, Thierry Murunga, Christopher Nikitas, Ishaan Patel, Victor Richmond, Kees Rodenburg, Neel Ruparelia, Arjun Taylor na Alessandro Tumiottoends…
Mratibu wa mashindano hayo, Alexander Mwaipasi alisema kuwa maandalizi yanaendelea vizuri na timu zaidi ya 15 zitashiriki katika mashindano hayo. “Timu nyingi zimetuma majina ya waogeaji wao na zipo tayari kwa mashindano,” alisema Mwaipasi.
No comments:
Post a Comment