HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 16, 2015

MSAADA WA MATIBABU UNAHIDAJIKA KWA DADA HUYU

Habari kaka,

Napenda kutumia fursa hii kukushirikisha habari ya kusikitisha kuhusu dada Joyce Mwambepo mkazi wa Sinde jijini Mbeya. Dada huyu mwenye umri wa 27 anaishi na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 pamoja na mwanaye mwenye umri wa miaka 4.

Kwa bahati mbaya mwezi April mwaka jana dada huyu alipata ajali ya kugongwa na gari ambayo hata hivyo haikusimama kumsaidia. Ila kwa msaada wa wasamaria wema alipelekwa hospitali ya raufaa mkoani Mbeya ambako alikaa kwa miezi mitatu bila kupata matibabu.

Katika uchunguzi wa awali ilibainika kuwan Joyce amevunjika miguu yote miwili hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia baada ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa Mbeya baada ya kudaiwa kukoswa shilingi 550,000/- za matibabu.

Hadi nakutana naye dada huyu alikuwa amelala nyumbani kwa bibi yake ambaye mlezi wake tangu akiwa na miaka minne baada ya wazazi wote wawili kufariki.

Hivyo nimejitahidi kufuatialia ili kujua mahitaji halisi lakini sikufanikiwa kumpata dakttari bingwa wa mifupa .Ili kumsaidia Joyce inatakiwa aanze process upya za matibabu kuanzia hapa Mbeya referral Hosp hadi Muhimbili.

Gharama za matibabu ni kama ifuatavyo
1. shilingi 300,000/- za kupima CT-SCAN
2. Shilingi 250,000/- za MRI
3. Usafri wa kutoka Mbeya-Dar kwa kukodi gari maalum 700,000/-
4. Gharama za msaidizi ambaye ni rafiki yake 200,000/-
5. Chakula (Mchele, Unga, Sukari, Maharage, Mafuta)
6. Gharama za matibabu (CT-SCAN&MRI) ni vipimo tu
7. Na mahitaji mengineyo wakiendelea kupata tiba

Asante sana kwa moyo wako wa kujitoa na Mungu atakubariki

Deo Kakuru Msimu
Msamaria mwema
0769 512 420

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad