HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, October 7, 2015

UHURU ONE YAZINDUA MFUMO WA KWANZA WA MAWASILIANO YA 4G DVNO LEO JIJINI DAR

 Meneja Mkuu wa  kampuni ya Tigo, Diego Gutierrez, akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kwenye mkutano kuhusina na kampuni ya Tigo kuanza kutumia mfumo wa kwanza Afrika wa mawasiliano ya 4G DVNO ikishirikiana na Uhuru One.
Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez akiwa na Mwenyekiti wa uhuru One Rajab Katunda wakati wa uzinduzi kuanzisha kutumia mfumo wa kwanza Afrika wa mawasiliano ya 4G DVNO ikishirikiana na Uhuru One.

KAMPUNI ya  Tigo na kampuni ya UhuruOne wameanzisha ushirikiano na kuunda mfumo wa utoajihuduma za kimtandao usiotumia miundombinu asilia ya mawasiliano (Data Virtual Network Operator – DVNO) na ambao utaiwezesha UhuruOne  kupanua upatikanaji wa huduma zake kwa kutumia teknolojia ya 4G. 

Aina hii ya mfumo wa mtandao ni ya kwanza barani Afrika.
Mfumo wa DVNO utaiwezesha UhuruOne  kusambaza taarifa za kimtandao  pamoja na mtandao wa data wa Tigo 4G LTE utakaowezesha  wateja wake  kutumia data  zilizowezeshwa kupitia kasi kubwa ya 4G.

Akitoa maoni yake kuhusu hili, Meneja Mkuu wa Tigo, Gutierrez alisema: “Hii ni mara ya kwanza barani kuwepo na ushirikiano wa aina hii ambapo Tigo inafurahia kufanikisha jambo hili kwa kushirikiana na UhuruOne. 

Kuzinduliwa kwa teknolojia ya 4G ni sehemu ya muendelezo wa mkakati wa Tigo kuboresha ubora huduma zake na kuwafikishia watu wengi zaidi huduma ya mawasiliano nchini.”

Aidha Mwenyekiti wa UhuruOne Rajabu Katunda alisema“tunaiona Afrika ikichipua  kiteknolojia, lakini kujumuisha  uwanda mpana wa mawasiliano na dijitali  kwenye uchumi wetu kutautendea uchumi wetu jambo ambalo litatuneemesha sisi wenyewe na kutuinua kimaisha. Hili ni jambo la kipekee na la kujivunia kwa UhuruOne ambayo imekuwa katika harakati za ubunifu kupitia mtandao wa intaneti tangu mwaka 2009 na pia ni mwanachama mwasisi wa  Umoja wa Dynamic Spectrum”.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad