HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, October 6, 2015

HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

STAR TV NEWS
Uongozi wa chama cha DP waitaka serikali kuchunguza kwa makini kifo cha mweneyekiti wa chama hicho, kufuatia sintofahamu iliyotanda. https://youtu.be/gDuTtHQHOLo
Tanzania yatajwa kupoteza kiongozi shujaa na mpenda haki kwa misingi ya sheria bila uvunjifu wowote kwa amani, Mchungaji Christopher Mtikila. https://youtu.be/ewjw2zURbWA
Mamlaka ya manunuzi ya umma PPRA yazifungia kampuni saba pamoja na wakurugenzi wake kushiriki zabuni za umma kufuatia ukiukwaji sheria ya manunuzi. https://youtu.be/5ftV1WUH0xM
Serikali yatarajiwa kufikishwa mahakamani kwa kile kinachodaiwa kuwa ukiukwaji wa haki za binadamu na kuminya uhuru wa habari na vyombo vya habari. https://youtu.be/28YJNS_VOKk
Mgombea wa CCM Dr.Magufuli aonya kuwa kuendelea kwa vitendo vya vurugu mkoani Arusha huenda vikaharibu heshima na sifa za mkoa huo. https://youtu.be/v_GZ_xl1x4c
Chama cha ACT wazalendo kimesema kinakusudia kufanya mageuzi makubwa katika sekta ya utalii nchini ili kuongeza fursa pamoja na mapato yatokanayo na sekta hiyo. https://youtu.be/YAZ2c8_X7QU

Azam tv news
Mgombea uraisi wa CCM Dr.Magufuli aahidi kufuata nyayo za hayati Moringe Sokoine kwa kufanya kazi kama yeye kwani aliuchukia Ufisadi. https://youtu.be/vWb6bzJEO0w
Wananchi waaswa kuendelea kuwa na imani na chama cha mapinduzi kwa kupigia kura madiwani,wabunge na raisi kutoka chama hicho ili wamalize miradi ya maendeleo. https://youtu.be/p5sC1oPtOP0
Hali ya sintofahamu yatanda kwa saa kadhaa baada ya wafuasi wa vyama vya ACT na CCM kukutana uwanja mmoja na kuzua vurugu. https://youtu.be/URXwAPnMnfw
Wizara ya afya na ustawi wa jamii yathibisha ugonjwa wa kipindupindu kuendea kwenye mikoa 9 hapa nchini.https://youtu.be/SenhbffWsb8
Raisi Jakaya Kikwete amaliza ziara yake nchini Kenya na kuhutubia bunge na baraza la seneti nchini humo.https://youtu.be/N75qPsGpZbU
Baadhi ya maeneo ya mkoa wa Arusha na Kilimanjaro yaendelea kuzizima kufuatia uwepo wa wagombea uraisi wa vyama vya CCM,CHADEMA na ACT. https://youtu.be/liwB2Pdhnj8

CH 10: Mwili wa aliyekua mwenyekiti wa chama cha Democratic Party Mchungaji Christopher Mtikila watarajiwa kuagwa kesho katika viwanja vya Karimjee. https://youtu.be/lKIONfwlJpo
Ch 10: Uongozi wa mahakama nchini wahimiza majaji wa mahakama kuu kuhakikisha kesi za uchaguzi zinatolewa hukumu kati ya miezi 6 hadi 8. https://youtu.be/J_R0Izrt_jY
CH 10: Mgombea urais kupitia tiketi ya CHADEMA Edward Lowassa aahidi kuzibiti tatizo la mgao wa umeme endapo ataingia madarakani. https://youtu.be/cKqgn1N6HHY
ch 10: Mgombea uraisi wa CCM Dr.Magufuli aahidi kufuata nyayo za hayati Moringe Sokoine kwa kufanya kazi kama yeye kwani aliuchukia Ufisadi. https://youtu.be/gIUBX8y6E80
CH 10: Nchi za Afika Mashariki zahitajika kuwekeza zaidi katika nishati endelevu ili iwe chachu ya maendeleo ya uchumi na ustawi wa jamii. https://youtu.be/uYomraBGkUI
CH 10: Serikali na benki ya CRDB yawekeana makubaliano yakutoa mikopo ya nyumba kwa watumishi ya umma wa nchini Tanzania. https://youtu.be/-DhwQcdoon0
Ch 10: Kuelekea pambano la kesho la soka Tanzania dhidi ya Malawi makocha wa timu hizo mbili waanza kutambiana ushindi wa timu zao. https://youtu.be/pj5GfiNkBrY
Ch 10: Kocha Jurgen Kloop aonekana ndiye kocha sahihi kwa Liverpool baada ya kocha Brendan Rodgers kufukuzwa kazi klabuni hapo. https://youtu.be/VB15YhaHCto

TBC: Mgombea wa urais Zanaibar kwa tiketi ya CCM awaomba wananchi wa mkoa wa Kaskazini A visiwani Zanzibar kuipa ridhaa CCM tena ili iwaletee maendeleo. https://youtu.be/s7uz7q3uDWo
Tbc: Mgombea mwenza wa CCM Samia Suluhu Hassan aanza mikutano yake ya kampeni mkoani Kigoma kwa ahadi ya kuboresha huduma za kijamii. https://youtu.be/XAa9owFaqr4
TBC: Makamu wa rais Dk. Bilal aweka jiwe la msingi la mradi mkubwa wa uzalishaji wa umeme wa upepo kusini mwa jangwa la sahara ujenzi kuanza hivi karibuni mkoani Singida. https://youtu.be/0rF7O7rnIDM

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad