HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 8, 2015

ZAIDI YA WANAFUNZI LAKI SABA 7.7 WANATARAJIWA KUFANYA MTIHANI WA KUMALIZA DARASA LA SABA SEPTEMBA 9 HADI 10 MWAKA HUU


Zaidi ya wanafunzi laki saba 7.7 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza darasa la saba katika vituo zaidi ya elfu 16 nchni nzima kuanzia Septemba 9 hadi 10 mwaka huu. 
 
Akizungumza na waandishi wa habari, Kaibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Tanzania Daktari Charless Msonde amesema kati ya wanafunzi hao wavulana laki tatu na  sitini na moja elfu sawa na asilimia 45.6, wasichana ni laki nne na kumi na nne elfu sawa na asilimia 53.4, ambapo masomo yatakayotahiniwa ni Kiswahili, Kiingereza, Sayansi, Hisabati na maarifa ya jamii. 
 
Amezitaka kamati za mitihani za mikoa na wilaya kuhakikisha taratibu za mitihani zinazingatiwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha vituo vya mitihani vinakuwa salama, hususani katika kipindi hiki ambacho baadhi ya viwanja vya shule za msingi vinatumiwa na vyama vya siasa kwa ajili ya kampeni za uchaguzi mkuu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad