Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donnan Mmbando
akizungumza na waandishi wa habari juu ya matumizi ya dawa katika Nchi
za Jumuiya ya Afrika Mashariki yawe na uwiano sawa na kuwa na kiwango
kinachokubalika Kimataifa. Amesema mamlaka husika inapaswa kusimamia na
wataalam wa dawa ili kuendana na soko la Jumuiya ya Afrika Mashariki,
leo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi
wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu jinsi namna wananchi watapata dawa zilizo
bora na salama zaidi kwa kutumia vigezo vya kikamataifa kwa kuwa
kuzingatia masharti yanayotolewa na Shirika la Afya Duniani. Amesema
Tanzania ni nchi ya kwanza kutoa uhamasishaji huu kwa wadau wazalishaji
na wasambazaji wa dawa na wote wanaojihusisha na biashara ya dawa na
kwamba hii ni jumuiya ya kwanza katika bara la Afrika kutekeleza
mpango wa kuwa na mifumo ya aina moja ya uthibiti wa dawa kwa Nchi za
Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Sehemu ya wadau wa dawa walio hudhulia kikao hicho leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donnan Mmbando na
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Hiiti Sillo wakiwa
katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donnan Mmbando na
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Hiiti Sillo wakifurahia
jambo baada ya kikao hicho (Picha na Emmanuel Mssaka)






No comments:
Post a Comment