HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, September 20, 2015

TMF KUWATUZA WAANDISHI KESHO

MFUKO wa Habari Tanzania utatoa kesho tuzo maalum tuzo kwa waandishi waliowezeshwa na TMF na kazi zao kuweza kuleta mabadiliko chanya. Hafla ya utoaji tuzo hizo itafanyika jijini Dar es salaam kesho tarehe 22 Septemba na itaambatana na maonyesho ya kazi hizo za kiuandishi.  Tukio hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali na watu mashuhuri kutoka kwenye taaluma ya uandishi wa habari pamoja na asasi za kiraia, wafadhili na serikali.

“Wakati Mfuko wa Habari Tanzania ukifikia tamati, tumeona kwamba ni muhimu kutambua juhudi za waandishi tuliowahi kuwawezeshwa. Waandishi wa habari wengi tuliowawezesha walikabiliana na changamoto nyingi katika kupata habari na kuweza kuuletea umma habari hizo. Mara nyingi walitishiwa maisha yao na kukabiliana na vitisho vya aina mbalimbali lakini walijitahidi kuandika habari zenye uwiano na zilizofanyiwa utafiti ipasavyo. Tunataka kutambua juhudi zao,” alisema Mkurugenzi wa TMF Ernest Sungura katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana.

Tuzo za TMF zilitangazwa kwa waandishi waliowezeshwa na TMF na walitakiwa kutuma kazi zao mwezi Julai 2015. 

Kwa mujibu wa Sungura, kazi zaidi ya 70 zilipokelewa kutoka kwa waandishi wa habari na taasisi za habari kutoka maeneo mbalimbali ya nchi. Matokeo ya mwisho ya uhakiki pamoja na tuzo zenyewe vitatangazwa kwenye maadhimisho ya miaka nane a TMF pamoja na utoaji tuzo tukio ambalo litafanyika kwenye ukumbi wa LAPF Millenium Towers.

Tangu kuanzishwa kwake, mradi wa TMF umekuwa ukisistiza na umuhimu wa kazi za uandishi katika kuleta uwajibikaji. Vigezo hivi vitatumika kuwapata wapokeaji tuzo. 

Sungura said: “Ni muhimu kuwapa motisha waandishi wa habari. Sherehe ya utoaji tuzoni sehemu ya maadhimisho yetu ya miaka nane ya mafanikio katika kuongeza uwajibikaji kwa kuimarisha sekta ya habari nchini. Tusingeweza kupata mafanikio haya bila ushirikiano wa wadau wetu katika sekta ya habari. 

Tukio hilo litaambatana na burudani kutoka kwa Mrisho Mpoto na Wahapahapa Band. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad