ARUSHA-Timu
ya maafande wa Jkt Oljoro inayoshiriki ligi daraja la kwanza Tanzania
bara inatarajia kuchuana vikali na ndugu zao timu ya Arusha FC katika
ufunguzi wa ligi maalum ya Nyerere cup inayotarajiwa kuanza kutimua
vumbi septemba 10 jiji Arusha.
Tiyari timu ya Arusha FC
na Jkt Oljoro zimethibitisha kushiriki michuano hiyo huku kila mmoja
akijitamba kuonyesha ubabe dhidi ya mwenzake na pia wakitumia mechi hiyo
kutambulisha wachezaji wao kwa wapenzi wa Soka wa jiji Arusha.
Mechi hiyo ya ufunguzi kati ya Oljoro na AFC itakayochezwa jioni katika uwanja wa Sheik Amri Abeid, ni kwa ajili ya kufungua michuano ya Nyerere cup itakayoshirikisha
Jumla ya timu Sita za vijana chini ya umri wa miaka 13, lengo kubwa
ikiwa ni kumuenzi muasisi wa Taifa hili Hayati Mwl, Julius K. Nyerere.
Akizitaja
timu shiriki katika ligi hiyo, mratibu wa maadhimisho hayo Bertha
Ismail alisema kuwa ni pamoja na Nyota Accademy, Future Star, Kijenge
Youth zingine ni Rolling stone, Young Life na Pallot.
“Maadhimisho
haya huwa yanafanyika Octoba 14 kila mwaka lakini kwa mwaka huu
tunafanya mwezi Septemba ili maadhimisho haya yasiathiriwe na zoezi la
Uchaguzi ambapo pamoja na kumuezi Muasisi wa Taifa letu lakini ligi hii
pia inalenga kuhasisha wananchi wafanye uchaguzi kwa amani bila vurugu
ili sekta ya utalii hapa nchini izidi kukua”
“Katika
maadhimisho haya yatakayofunguliwa na mkurugezi wa jiji la Arusha Iddi
Juma yana “kauli mbiu ni Uchaguzi wa amani 2015: Taifa Moja kwa
Maendeleo ya utalii” ambapo wadau mbali mbali wa maendeleo ya nchi yetu
na utalii kwa ujumla watahudhuria ufunguzi na kilele ambayo ni septemba
19 na atakaefunga ni mkurugenzi wa hifadhi ya Taifa (TANAPA) Allan Kijazi”


No comments:
Post a Comment