HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, September 21, 2015

MAADHIMISHO YA CP DAY KUFANYIKA OKTOBA 7 MWAKA HUU JIJINI DAR

Makamu  Mwenyekiti wa Chama cha Wazazi Watoto wenye Ulemavu wa mtindio wa Ubongo na akili na Viungo Tanzania (CHAWAUMAVITA) Hillar Said  akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya Maadhimisho ya mwaka  huu maadhimisho hayo yatakayofanyika Oktoba 7 mwaka huu katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jjijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadicki, kulia ni Katibu (CHAWAUMAVITA) Mwanahamisi Hussen

Mwenyekiti  huyo wa (CHAWAUMAVITA) , amewaomba wanachama kuchangia ili kufanisha zoezi la Maadhimisho hayo.


Na Dotto Mwaibale
CHAMA cha Wazazi wa Watoto Wenye Ulemavu wa Mtindio wa Ubongo, Akili na Viungo (Chawaumavita) kimewataka wakina baba kuacha tabia ya uoga ya kukimbia majukumu pindi wanapopata watoto wenye ulemavu.

Katika hatua nyingine chama hicho kimewaomba wagombea wa vyama mbalimbali vya siasa kuzungumzia namna gani watasaidia walemavu katika mikutano yao.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Watu na Watoto Wenye Mtindio wa Ubongo ambayo huazimishwa kila mwaka ifikapo Oktoba 7. Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Hilal Saidi, alisema watoto wenye matatizo hayo wanapaswa kusaidia badala ya kuwatenga.

Alisema kuwa  katika tafiti walizofanya wamegundua kuwa wanaume wengi ni waoga wa majukumu pindi wanapopata watoto wenye ulemavu hadi kupelekea kukimbia famia zao.

"Wanaume wengi waoga wa majukumu hasa anapozaliwa mtoto mwenye ulemavu, wanaona kuwa ni mkosi mkubwa na kuanza kupata msukumo katika familia yake kuachana na mkewe hivyo anateleleza familia huku mwanamke akibaki peke yake" alisema Said

Hata hivyo alisema ulemavu umegawanyika katika makundi matatu ambayo ni  ni ulemavu wa akili,mtindio wa ubongo na viungo.

Alisema watoto wenye ulemavu wa viongo na mtindio wa ubongo wanaweza kupatiwa matibabu hali yao ikawa sawa kushiriki katika katika elimu na kufikia malengo yao.

Hivyo aliwataka wakina baba na familia kwa ujumla kutowafungia ndani watu wenye ulemavu na badala yake kuwapeleka katika vituo vya afya kwaajili ya matibabu na miili yao ikatengemaa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad