HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, August 3, 2015

WANAZUONI WA KIISLAAM WATAKA AMANI KATIKA UCHAGUZI MKUU

 Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
Umoja wa Wanazuoni wa Kiislaam nchini umetaka kuwepo kwa amani katika uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Umoja huo , Mwenyekiti wa Kamati ya Usuluhishi,Suleiman Kilemile amesema nchi nyingi zimeingia katika machafuko kutokana na uchaguzi hivyo nchi yetu isiingie huku.

Amesema kauli za viongozi  wa siasa za hivi karibu katika michakato ya kuelekea uchaguzi zinaweza kuharibu amani yetu hivyo ni wakati wa  umefika kuweza kuangalia lugha za kutumia katika kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba.

Kilemile amesema amani iliyopo lazima iendelee kulindwa katika kujiepusha na machafuko ambayo nchi zingine zimeingia kutokana na siasa.

Amesema miaka mitano ya mwisho katika nchi ya Misri wanawinda amani ya watu kutokana na maumivu  wanayoipata ambapo nchi hiyo ilikuwa ya amani. 
 Mwenyekiti wa Umoja wa Wanazuoni Tanzania Shehe Suleiman Kilemile akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo katika Ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO.
 Mwenyekiti wa kamati ya usuluhishi wa Umoja wa wanazuoni wa Kiislam tanzania, Ally Said Bassaleh akizungumza na waandishi katika ukumbi wa habari Maelezo jijini Dar es Salaam leo.
Waandishi wa habari wakimsikiliza  Mwenyekiti wa Umoja wa Wanazuoni Tanzania Shehe Suleiman Kilemile wakati akizungumza kuhusiana na amani ya nchi wakati wa uchaguzi mkuu utakao fanyika Oktoba mwaka huu.  
Picha na Avila Kakingo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad