Naibu Mkurungenzi wa Masuala ya watumiaji Huduma za Mawasiliano wa TCRA, Issac Mruma akizungumza na Baadhi ya wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya (Bongofleva) (hawapo pichani) juu ya matumizi ya mitandao ya kijamii, huku akiwataka kujilinda dhidi ya Mbinu za kitapeli,wizi na udanganyifu kupitia mitandao ya Mawasiliano, wakati wa semima ya siku moja iliyofanyika leo kwenye Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jiji Dar es Salaam.
Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy akizungumza na Baadhi ya wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya (Bongofleva) (hawapo pichani) wakati wa semima ya siku moja iliyofanyika leo kwenye Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jiji Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa semina hiyo leo Makao Makuu ya Mamlaka ya Mawasiliano(TCRA) Tanzania Jiji Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka.
No comments:
Post a Comment