HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, August 11, 2015

SSRA katika maonesho ya Sherehe ya wakulima (NANE NANE) Mkoani Morogoro

Afisa uhusiano mwandamizi Bw. Fulgence Sebera akitoa maelezo ya shughuli za Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kwa Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Mhe. Majid Mwanga (wa tatu kulia) aliyeambatana na viongozi wengine wa TASO walipotembelea banda la SSRA katika sherehe za maonesho ya wakulima Nanenane yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere mkoani Morogoro.
Maafisa waandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) wakisikiliza kwa makini maoni ya mdau wa jamii ya wafugaji alipotembelea banda la Mamlaka katika maonesho ya Nanenane mkoani Morogoro.
Mch. Vernon Fernandes (aliyekaa) alipotembelea banda la SSRA katika maonesho ya Nanenane Morogoro, kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji Bi Sarah Kibonde Msika akifuatiwa na mwanasheria mwandamizi Bw. Omar Sururu Khalfan, kushoto ni Afisa matekelezo Bw. David Lyanga.
Mkuu wa kitengo cha uhusiano na uhamasishaji Bi Sarah Kibonde Msika wa kwanza kushoto akitoa maelezo ya masuala ya Hifadhi ya Jamii kwa wadau waliotembelea banda la SSRA, akifuatiwa na afisa matekelezo Bw.David Lyanga na afisa uhusiano mwandamizi Bw. Fulgence Sebera katika maonesho ya Nanenane Morogoro.
Maafisa wa Mamlaka wakikabidhi zawadi ya Mfuko wa SSRA kwa mdau aliyetembelea banda la Mamlaka katika maonesho ya Nanenane mkoani Morogoro.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad