HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, August 1, 2015

KUMBUKUMBU

Mpendwa Mama Rhoda Cleopa Msuya
Daima tutakupenda kamwe hatutokusahau.
Ni Miaka kumi tangu ulipotangulia

Tumebaki na kumbukumbu za mapenzi yako ya dhati na wema wako
Tumekukumbuka leo, jana, juzi na siku kabla yake

Tunakukumbuka moyoni na kila tunapotaja jina lako

Kumbukumbu zetu kwako haziwezi kuelezeka

Tumebaki na kumbukumbu ya tabasamu lako na picha yako

Ni kumbukumbu za upendo wako ndio zinatupa nguvu ya kuendelea mbele

Daima utabaki katika mioyo yetu

Uko Katika Ufalme wa Mungu, Tunakuombea upumzike kwa amani.


Unakumbukwa daima na mume wako Cleopa, watoto wako George,John,Joyce, Job, Naanjela.
Wakwe, Onesmo, Khadija,Mercy,Mary na Yoko, wajukuu, ndugu na marafiki.

Misa maalum ya kumbukumbu ya wapendwa wetu Mama Rhoda Cleopa Msuya na Geoffrey Cleopa Msuya itafanyika Tarehe 9 August 2015 kwenye kanisa la Azania Front Cathedral saa tatu na nusu asubuhi,
Wote mnakaribishwa.

“kuwakumbuka wenye haki huwa na baraka” Mithali 10:7

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad