MAKAMU Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazee Zanzibar (JUWAZA), Mwadini Kutenga Haji akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa vyakula kwa wazee wa Zanzibar uliotolewa na kampuni ya simu ya Zantel.
WAZEE mbali mbali wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa msaada wa vyakula uliotolewa na kampuni ya simu ya Zantel , makabidhiano hayo yalifanyika Kibanda maiti.
MKURUGENZI wa Biashara wa Kampuni ya simu ya Zantel ofisi ya Zanzibar, Mohammed Mussa akizungumza katika hafla ya kukabidhi misaada ya vyakula iliyotolewa na kampuni hiyo kwa wazee mbali mbali wa Zanzibar.
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto, Msham Juma Khamis akihutubia wazee mbali mbali waliokua katika hafla ya kukabidhiwa msaada wa vyakula vilivyotolewa na kampuni hiyo. Kulia Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni ya simu ya ZANTEL, Mohammed Mussa na kulia Makamu Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazee Zanzibar (JUWAZA), Mwadini Kutenga.
NAIBU Katibu Mkuu, Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii , Vijana , Wanawake na Watoto, Nd. Msham Juma Khamis akimkabidhi msaada , Pili Ahmada wakati wa makabidhiano ya msaada wa vyakula uliotolewa na Kampuni ya simu ya Zantel kwa wazee mbali mbali wa Zanzibar, kulia Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel Zanzibar, makabidhiano hayo yalifanyika jana Kibanda maiti.
MZEE Hussein Abdalla akipokea msaada wa vyakula kutoka kwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii , Vijana , Wanawake na Watoto, Nd. Msham Juma Khamis , msaada huo ulitolewa na kampuni ya simu ya Zantel, kulia Mkurugenzi wa Biashara wa Zantel Zanzibar, makabidhiano hayo yalifanyika jana Kibanda maiti. (Picha na Haroub Hussein).
No comments:
Post a Comment