HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, July 28, 2015

MH. LOWASSA ATINGA RASMI UKAWA JIONI HII

 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe (kushoto) akimkabidhi rasmi kadi ya uwanachama wa CHADEMA, Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa mara baada ya kujiunga na Chama hicho jioni hii kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Bahari Beach, Jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Freeman Mbowe (kushoto) akimpongeza Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa mara baada ya kujiunga na Chama hicho jioni hii kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Bahari Beach, Jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakionyesha kazi zao za CHADEMA mara baada ya kujiunga rasmi jioni hii.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa akiingia kwenye ukumbi wa mikutano ndani ya hotel ya Bahari Beach jijini Dar,kwenye mkutano wa Wanahabari jioni ya leo.
 Mh.Lowassa akiingia kwenye Hoteli Bahari Beach  kwa ajili ya kutangaza adhima yake ya kujiunga na UKAWA. Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa ametangaza kujiunga rasmi na Umoja wa Katiba (UKAWA) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) .
 Mh.Lowassa akiwa na viongozi wa UKAWA  katika Hoteli ya Bahari Beach Hoteli jijini Dar es Salaam jioni ya leo mara baada ya kutangaza rasmi azma yake ya kujiunga na ukawa.
 Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema,Freeman Mbowe akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa katika Hoteli ya Bahari Beach Jijini Dar es Salaam jioni hii alipokuwa akitangaza azma yake ya kujiunga na UKAWA kupitia chama cha CHADEMA.
Mh.Waziri Mkuu Mstaafu,Edward Lowassa akiteta jambo na Mwenyekiti Taifa wa Chama Cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba  katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam.

1 comment:

Post Bottom Ad