Meneja wa tawi la LG Mtaa wa Nkurumah, Yasin Lodhi, (kulia) akikabidhi zawadi ya Microwave kwa Bi. Hidaya Kapera, (kushoto) mara baada ya mteja huyo kufanya manunuzi ya bidhaa za kisasa ndani ya banda la LG katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara maarufu kama Sabasaba.
Mkufunzi
mwandamizi toka kampuni ya LG, Elizabeth Morris, (Kulia) akimpa mkono
na Bw. Festo Sakaya (kushoto) baada ya mteja huyo kujinunulia friji la
kisasa ndani ya banda lao la maonyesho ya Sabasaba ambapo baada ya
kufanya manunuzi alizawadiwa microwave ya bure, ya LG. Kampuni hiyo ipo
kwenye promosheni ya punguzo la bidhaa zake kwa asilimia 15 kwa msimu
huu wa sabasaba na ramadhani. Katikati ni meneja wa tawi la LG Mtaa wa
Nkurumah Bw. Yasin Lodhi.
Mkufunzi
mwandamizi toka kampuni ya LG, Elizabeth Morris, (Kushoto) akiwaonyesha
waandishi wa habari moja ya microwave ambayo inatolewa kama zawadi kwa
wateja wanaonunua friji za kisasa za LG. Tukio hilo lilifanyika katika
banda la LG ndani ya viwanja vya maonyesho ya 39 ya biashara kimataifa
maarufu kama Sabasaba, wa pili kushoto ni meneja wa tawi la LG Mtaa wa
Nkurumah ,Yasin Lodhi .
Bw.
Festo Sakaya akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupokea
zawadi ya Microwave ya kisasa toka LG ambayo aliipata baada ya kufanya
manunuzi ya friji la kisasa ndani ya banda la LG wakati wa maonyesho ya
39 ya biashara kimataifa maarufu kama Sabasaba.
No comments:
Post a Comment