HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 10, 2015

wagonjwa wa vikope kufanyiwa upasuaji

Na. Catherine Sungura, MOHSW-Arusha

Zaidi ya wagonjwa elfu arobaini wanaougua ugonjwa wa vikope unaotokana na trakoma wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa macho katika mikoa sita nchini Tanzania kwa muda wa miaka mitano.

Hayo yamezungumzwa jana jijini hapa na Mratibu wa Mpango wa kudhibiti magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele dkt. Upendo Mwingira wakati akiwasilisha mada kwenye mkutano wa nne wa kazi kati ya wizara na wadau wanaofadhili mpango huo Upasuaji huo unafadhiliwa na shirika la msaada la Uingereza (DFID) pamoja na mfuko wa msaada wa Malkia Elizabeth (QETF) katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Arusha, Manyara, Pwani pamoja na Dodoma.
Dkt. Mwingira alisema tathimini iliyofanyika nchi nzima inakadiriwa kuwa na wagonjwa wa vikope wapatao laki moja, hivyo ili kudhibiti ongezeko la upofu nchini ,serikali imeanza kufanya upasuaji wa wagonjwa hao.

“Watu wenye matatizo ya vikope hupata usumbufu wakati kope zikigusa kioo cha jicho na mwishowe kupofuka,hivyo njia hii ya upasuaji itawasaidia kurudi katika hali ya kawaida na kujisaidia katika shughuli zao binafsi na zile za maendeleo ya Taifa kwa ujumla” alisema Ugonjwa wa vikope husababishwa na bakteria aina ya “Chlamydia Trachomatis” wanaosambazwa na inzi na pia kwa njia ya kuchangia taulo au vitambaa na kugusa macho ya mtu anayeugua ugonjwa huo , hivyo usipotibiwa mapema unaweza kusababisha upofu.

Mkutano huo unawajumlisha wadau kutoka nchini Washington DC, Liverpool, Geneva pamoja na baadhi ya waratibu wa mpango huo toka mikoa ya Tanzania bara.
Dkt.Upendo Mwingira akimkabidhi zawadi ya kinyago mwakilishi mkazi wa shirika la IMA World Health Jim Cox anayemaliza muda wake nchini.IMA World Health ni moja ya wadau wa mpango huo.
Dkt. Jeremiah Ngondi kutoka RTI International ambayo inatekeleza Mpango wa Taifa Kudhibiti Magonjwa yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele, akizungumza katika Mkutano huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad