HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, June 27, 2015

USHIRIKI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII KWENYE MAONYESHO YA 39 YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA DARES SALAAM

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
 TANGAZO KUHUSU USHIRIKI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII  KWENYE MAONYESHO YA 39 YA  BIASHARA YA KIMATAIFA YA DARES SALAAM
  1. Wizara ya Maliasili na Utalii inashiriki kwenye Maonyesho ya 39 ya  Biashara ya Kimataifa ya Dares Salaam (Saba Saba) yatakayofanyika katika viwanja vya Mwalimu Julius.K.Nyerere,  Barabara ya Kilwa kuanzia tarehe 28 Juni hadi 8 Julai, 2015.
  2. Karibu kwenye Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii ujionee na kuelimika kuhusu shughuli za Utalii,  Ufugaji Nyuki, Uhifadhi wa Misitu, Malikale na Wanyamapori.
  3. Safari za kutembelea Hifadhi za Mikumi na Saadani kwa gharama nafuu zitakuwepo
  4. Aidha, Wizara itachezesha bahati nasibu ambapo mshindi atazawadiwa safari ya kwenda kutembelea Hifadhi ya Mikumi au Saadani.
  5. Pia, Utapata fursa ya kuwaona wanyamapori hai kama vile Chui, Mamba, Nyoka, Ndege wa aina mbalimbali pamoja na mfalme wa pori SIMBA.
Karibuni Wote
“Unganisha Uzalishaji    na Masoko ”




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad