HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 10, 2015

UHARIBUFU KATIKA BARABARA YA VIWANDANI, CHANG'OMBE JIJINI DAR

 Hivi ndivyo hali ilivyo katika barabara hii ya Viwandani, Chang'ombe jijini Dar es salaam. uharibufu huu wa barabara umetokana na Mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha maeneo mengi hapa nchi majuma kadhaa yaliyopita. Cha ajabu katika eneo hili bado maji ni mengi sana yametuama na huku uharibifu mkubwa wa barabara ukiendelea. Mzee wa Mtaa kwa Mtaa alibahatika kuzungumza na wadau kadhaa waliopo jirani na eneo hilo, ambapo walisema kuwa kuja kwa Dimbwi hilo ni kutokana na kutokuwepo kwa sehemu ya kusafirishia maji hayo kutokana na ujenzi holela wa Maghala na Viwanda vilivyolizunguka eneo hilo, hali inayopelekea kuwepo kwa adha hiyo kwa sasa. Je ni kweli kwamba ujenzi holela katika maeneo haya unapelekea kujaa kwa maji haya barabara??? Wataalam wa barabara tunaomba majibu. Picha zote na Othman Michuzi.
 Ile kauli ya "Kufa kufaana" ndiyo inayotumiaka hivi sasa katika eneo hili, kwani kuna baadhi ya vijana ambao wanaombea maji haya yaendelee kuwepo ili na wao wajipatie chochote kitu ili siku zisonge mbele. Pichani ni mmoja wa vijana hao akiiongoza moja ya gari kupita katika eneo salama bila kukwama, ambapo ujira wake ni kuanzia shilingi Elfu moja na kuendelea kutegemena na ubinaadamu wako.
 Kazi ikiendelea ya kuyapitisha magari katika maeneo salama.
 Kuna ambao ni wazoefu wa eneo hilo, wao wanapita kwa maarifa yao na hawatoi hata mia.
 Huyu alijaribu kupita lakini alikwama mpaka pale alipokuja mtaalam wa njia na kumuonyesha kwa kupita.
Sehemu ya Madhara katika barabara hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad