Nianze makala hii kwa kupongeza jitihada za dhati za serikali ya awamu ya Nne katika uwekezaji wake kwenye sekta ya TEHAMA Nchini. Ni wazi kabisa nchi yetu imepiga hatua kubwa katika maswala ya TEHAMA kulinganisha nan chi nyingi Afrika. Mifano michache ni pamoja na kuhama kutoka analogia kulekea Digitali, Mkonge wa taifa, Kupatikana kwa Khala Mtandao la taifa, kuaandikisha upigaji kura kimtandao na mengineyo mengi.
Aidha, Jitihada kama vile kupatikana kwa sharia mtandao, kupatikana kwa vitengo vinavyo shughulikia uhalifu mtandao, wakala za serikali mtandao na mengineyo yamekua ni hatua ya kipekee iliyoweza kutoa matumaini kwa watanzania kutoka kwa serikali ya awamu hii ya Nne inayo ongozwa na Dk. Jakaya Kikwete.
Jitihada hizi njema naona bado kuna ya kufanyika zionyeshe matunda na zibaki salama kwa muda mrefu. Nimeyasema hayo kufuatia kauli yangu niliyoitoa, Nilipo sema serikali ina jukumu la kuwekeza zaidi katika maswala ya usalama mitandao ili kuweza kubakisha salama jiihada hizi za TEHAMA kwani isipo fanywa hivyo kuna hatari kubwa mbele yetu kimtandao iyakayo pelekea jitihada hizi kuingia dosari kubwa.
Hatari za kimtandao zitakazo pelekea kuathiri kwa kiasi kikubwa uchumi wetu, siasa zetu, tamaduni na jamii yetu kwa kwa ujumla wake. Napo zungumzia uchumi nipamoja na upotevu mkubwa wa fedha unaosababishwa na uhalifu mtandao ulio athiri taasisi za fedha na mawasiliano nchini. Kumekua na wimbi kubwa la wizi wa fedha kimtandao hii ni mjumuisho wa pesa kutoka mabenki pamoja na pesa zinazo potea kutokea kwenye miamala ya simu.
Moja ya changamoto iliyo sikika kwenye kikao nilichoshiriki kilicho husisha nchi ya ujerumani na Tanzania ni pamoja na lalamiko kutoka kwa mshiriki kuelezea kua kupitia mtandao alipoteza pesa zake na kumekua na ugumu kuzipata pesa hizo. Nilitolea ufafanuzi hilo kwa kueleza kua tatizo ni kubwa na kama hakuna jitihada za dhati kudhibiti hili basi kuna hatari ya uchumi wetu kupitia uhalifu huu mtandao kuporomoka.
No comments:
Post a Comment