HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, June 2, 2015

TAARIFA YA KUBADILIKA KWA MUDA WA KUONDOKA TRENI YA DELUXE KUANZIA JUNI 7, 2015!

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unafuraha kuwatangazia abiria wote na wananchi kwa jumla  kuwa kutokana na sababu za kiufundi ikiwemo maoni ya wadau na wateja treni ya deluxe itaondoka Dar es Salaam kila Jumapili saa 2 asubuhi badala ya saa 2 usiku.

Kwa kubadilisha muda wa kuondoka na kuwa saa 2 asubuhi abiria wa treni ya deluxe watalala njiani kwa usiku mmoja tu.
Kwa vile treni hiyo itakuwa inawasili jioni kituo cha mwisho Kigoma au Mwanza hivyo basi nayo imepangiwa kuondoka siku inayofuatia saa 2 asubuhi pia!

Uongozi wa TRL siku zote ni sikivu unasikiliza maoni ya wateja wake kuhusu utoaji huduma wenye kuridhisha na wenye  ufanisi!

Atakaye soma taarifa  hii amwarifu na mwenziwe!

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Elias Mshana 
TRL Makao Makuu,
Dar es Salaam.
Juni 02, 2015.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad