Na. Aminiel Aligaesha (MNH)
Hospitali
ya Taifa Muhimbili (MNH) imezichachafya taasisi 84 zilizoshiriki
maonyesho ya wiki ya Utumishi wa Umma kwa kutwaa tuzo mbili kati ya tano
maalum zikiashiria kuwa
mshindi wa kwanza kwa kila tuzo. Tuzo ya kwanza ni ya ubunifu katika
kutoa huduma iliyokuwa ikitaka taasisi kuwa na ubunifu ama wa kuiga
(adoption) au asili (origin) na ambao haujawahi kufanyika hapa nchini na
ubunifu huo uwe umeleta tija katika utoaji huduma
eneo la kazi.
Katika
tuzo hii MNH imeshinda kwa kubuni njia mbadala ya kulea watoto
waliozaliwa kabla ya wakati (njiti) kupitia njia ya KANGAROO. Ubunifu
huu uliigwa kutoka nchi za Afrika
Magharibi na Afrika ya Kusini ambao walifanya utafiti kwa kumsoma
KANGAROO anavyolea watoto wake akiwa amewakumbatia na kuonyesha
mafanikio makubwa. Kwa misingi hiyo walionekana kufaulu ambapo vifo vya
watoto waliozaliwa kabla ya wakati vilipungua ukilinganisha
na wale wanaolelewa kwenye incubators. MNH ilianza mpango huu mwaka
2002 na tayari umeonyesha mafanikio makubwa sana ambapo tayari Hospitali
ya Lutheran Hydom iliyoko Arusha nayo imefundishwa na watalaam wetu
kutumia njia hii nayo ikafanikiwa.
Tuzo
ya pili iliyonyakuliwa na MNH ni tuzo ya banda bora kuliko yote wakati
wa maonyesho ambayo vigezo vyake pamoja na mambo vigezo vingine ni uwezo
wa washiriki husika
kujua taaluma yao, uwezo wa kuelezea huduma zinazotolewa na taasisi
wanayofanyia kazi, unadhifu katika banda na huduma bora kwa wateja.
Maonyesho
ya Wiki ya Utumishi wa Umma yalijumuisha taasisi 84 zilishiriki
kushindania tuzo nne ambazo ni (Tuzo ya Ubunifu, Tuzo ya Taasisi/Wizara
Inayosimamamiwa kwa Mjibu
wa Utawala Bora, Tuzo ya Uwezeshaji Akina Mama, Tuzo ya Mpango wa
Wafanyakazi Wanaoishi na VVU Mahali pa kazi. Aidha kati ya taasisi hizo
ni taasisi 42 ambazo zilishindanishwa kwenye Tuzo ya Tano ya Banda
Bora.
Kwa
misingi hiyo, MNH imezigaraza taasisi 42 zilizojitokeza kugombea nafasi
hiyo ikiziongoza ambapo tuzo hutolewa kwa washindi wa kwanza hadi wa
tatu. Aidha MNH imeziongoza
pia 84 kwenye nafasi ya kwanza kwenye tuzo ya ubunifu. Hii
inadhihirisha MNH ipo juu taasisi hizi haziiwezi, haikamatiki. Katika
tuzo ya Taasisi/Wizara Inayosimamamiwa kwa Mjibu wa Utawala Bora, MNH
imepata nafasi ya 8 kwani kila tuzo imetoa fursa angalu
ya kutambua taasisi 10.
Fuatilia habari katika picha:
Dkt. Bashir Nyangasa, Daktari Bingwa wa Upasuaji Moyo akifurahi baada ya kukabidhiwa tuzo ya Ubunifu
Baada
ya kupata tuzo mbili. Kutoka kushoto ni muuguzi kutoka chumba maalum
cha kujifungulia Anna Danfold ambaye alikuwa akielezea dakika ya dhahabu
ya kuokoa maisha
ya mtoto mara tu anapozaliwa. Anayefuatia ni Muuguzi Rose Silaa ambaye
ni Mkuu wa Kitengo cha Utunzaji wa Watoto kwa Njia ya Kangaroo
akionyesha mtoto anavyotunzwa kwa njia hiyo.
Wakashindwa kuzuia furaha zao hapa Washiriki wa MNH wakasakata dansi baada ya kupokea tuzo mbili
Wakapata picha ya pamoja kabla ya kuelekea Muhimbili kukabidhi kikombe kwa Mkurugenzi Mtendaji wao aliyewatuma
Wakawasili Muhimbili kwa mbwembwe
Juu
na chini ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili
akipokea vikombe kutoka washiriki wa maonyesho. Juu ni Muuguzi Nemganga
Kizegha na chini
Dkt. Bashir Nyangasa
Msitari
wa mbele ni baadhi ya Wakurugenzi wa MNH kwa pamoja wakiwa na nyuso za
furaha katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki
Mkurugenzi
wa Teknohama Bw. Modou Gaye akipokea tuzo hizo na kuyaweka Ofisi ya
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili
No comments:
Post a Comment