MHANDISI mashuhuri
George Mulamula (Pichani )ameipongeza programu mpya ya Airtel Tanzania
ijulikanayo kama “Airtel Fursa” inayowawezesha vijana kiuchumi ikiwemo
kuwapa mbinu mbalimbali zitakazowasaidia kupata maendeleo zaidi katika shughuli
zao.
Kama mmoja wa jopo la
washauri ambaye atachagua vijana watakaotimiza vigezo vya kuweza kuingia
katika mpango wa Airtel Fursa.
"Hii ni nafasi
nzuri ya kuleta mabadiliko, kuhamasisha vijana na kuwasaidia kujijenga
kibiashara endelevu na ninapenda kuwapongeza Airtel kwa ajili ya mpango
huu," alisema Mulamula.
Bwana Mulamula
aliahidi kufanya kazi kwa karibu na Airtel pamoja na jopo la washauri
katika kuhakikisha wanachagua na kuwapa mafunzo walengwa wa Airtel Fursa
ikiwa ni pamoja na kuwasaidia kuweza kutumia techonologia ya habari
yaani ICT kama nyenzo muhimu itakayowawezesha kuleta ufanisi katika
shughuli zao za uzalishaji na kiuchumi. Akiamini kuwa vijana
watakaofaidiaka na Airtel fulsa watahamasisha na kuongoza katika kuleta
mabadiiko kwenye jamii zao huku akihakikisha mpango huu unakuwa na mafanikio
makubwa kwa walengwa na kuwa na mvuto kwa vijana wengine .
Mhandisi Mulamula ni
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dar Teknohama (ICT) Business Incubator (DTBi) kwa
ajili ya ujasiriamali katika Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), analeta
uzoefu wa kutosha katika mpango huu wa Airtel fursa kwenye nyanja ya
ujasiriamali na kukuza biashara zinazoanza.
Yeye ni mshauri na
mwalimu kwa wajasiriamali. Amekuwa akisaidia kuinua vipaji vya watu mbalimbali
hapa nchini na nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na katika mkutano wa kimataifa wa
ujasiriamali nchini Moscow, Durban na Nairobi kwa ajili ya maonyesho ya Afrika.
Pia ni Mjumbe wa Bodi ya Demeter nchini Boston USA na pia Mjumbe wa Bodi ya
XPrize nje ya California, Marekani.
“Mpango huu unatafuta
vijana wenye kiu, nguvu na utayari wakupata wanachokiamini na kukihitaji, wenye
uwezo wa kuzipitia changamoto na kufikia matarajio waliojiwekea na wakati
huohuo kubadilisha maisha yao” aliongeza
Airtel Fursa
inawalenga vijana wenye umri kati ya miaka 18-24 ambao ni watanzania waishio
nchini Tanzania. Vijana hao ni lazima wawe wamiliki wa biashara ndogondogo,
wenye hali ya ushindani na kuheshimu biashara zao. Maelfu ya vijana watapata
mafunzo kupitia warsha mbalimbali na kupatiwa vitendea kazi vitakavyo boresha
biashara zao.
Hii inajumuisha
mafunzo katika usimamizi wa fedha, mikopo, faida za kuwa na akaunti ya benki na
usimamizi wa biashara kwa ujumla
Wanaotaka kujiunga
wanapaswa kutuma ujumbe mfupi kwenda 15626 ukiambatanishwa na taarifa
zifuatazo;- jina, umri,aina ya biashara, mahali na namba ya simu. Airtel Fursa
pia inakaribisha mapendekezo ya vijana wenye vigezo husika.
Maombi yanaweza
kutumwa pia kwa njia ya barua pepe airtelfursa@tz.airtel.com
au tovuti ya Airtel. Maombi yaambatanishwe na jina, umri, aina ya biashara,
mahali, namba ya simu na sababu ya kusaidiwa kibiashara.
No comments:
Post a Comment