Katibu mkuu wa Wizara ya Sayansi Pro. Patrick Makungu na Md of Huawei Tanzania Bw. Zhan Yongquan anayeshuhudia ni balozi wa china nchini Tanzania, Waziri wa Mawasiliano Sayansi na technolojia na waziri wa afya wa Zanzibar Bw kombo.
Waziri wa Wizara ya Sayansi pro. Makame Mbawara akielezea Data Center iliyojengwa hapa Tanzania . Pembeni yake ni Director wa ICT Dr. Ally Simba
Mr. Jiang Xin (Product Manager wa Huawei Enterprises) akielezea Data Center.
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Huawei
Tanzania Wakishirikiana Na Wizara Ya Mawasiliano, Sayansi Na Teknolojia waanda
Kongamano Lao La Kwanza La Huawei Cloud Conference Nchini Tanzania.
[Dar
es Salaam, Alhamisi 18 Juni 2015] Kampuni
ya Huawei Tanzania ikishirikiana na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na
Teknolojia leo hii wameandaa kongamano la kwanza la sekta ya TEHAMA (ICT) ijulikanayo
kama Huawei Cloud Conference kwenye ukumbi wa Julius Nyerere International
Convention Centre (JNICC).
Kongamano hili liliwakutanisha wadau
wote wa TEHAMA (ICT) nchini, wakiwemo wa serikali na wa sekta binafsi na lilizinduliwa
na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Balozi
wa China nchini Tanzania Bw. Lv Youquin, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi
na Teknolojia Prof Patrick Makungu pamoja na usimamizi wa makampuni shirika ya
Huawei Tanzania kutoka; Airtel, Viettel, Tigo, Vodacom, na TTCL.
Katika Kongamano hilo la mada
“Rahisisha Teknolojia, Rahisisha Biashara” ilizungumziwa hali ya sasa ya sekta
ya TEHAMA, sera zake pamoja na kupanga jinsi ya kuiendeleza sekta hii nchini
ili kufikia malengo ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ya millenia
ya 2025 ambayo ni kuendeleza Tanzania kupitia TEHAMA.
Katika kongamano hili kampuni ya
Huawei Tanzania (ambao ni wabunifu wakubwa wa bidhaa na huduma za TEHAMA)
pamoja na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia walitia sahihi mkataba
wa makubaliano kati yao huku ikiipa nafasi kampuni ya Huawei Tanzania kua moja
ya washauri wa mambo ya TEHAMA nchini.
Baada ya kutia sahihi, Kampuni ya Huawei
Tanzania ilielezea mipango yake ya kuendeleza na kukuza mawasiliano nchini
Tanzania kwa kukuza sekta ya TEHAMA na kutoa elimu serikalini, mashuleni na kwa
wananchi wote kwa ujumla kuhusu sekta iyo.
Tanzania imekua ikifanya kazi kwa karibu sana na Kampuni
ya Huawei Tanzania na kwa mda wote
kampuni hii imeshirikiana na wizara kwa karibu sana. Utiaji sahihi wa
makubaliano ya kushirikiana katika shughuli za TEHAMA ni ushuhuda tosha wa
jinsi Huawei Tanzania inavyojali sekta ya TEHAMA nchini na itaendeleza kukuza
teknolojia hiyo nchini.
Akizungumza
katika Kongamano hilo, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Technolojia, Prof.
Makame Mbarawa alisema, “TEHAMA inachangia sana katika maendeleo ya Uchumi ya nchi
kwani inawezesha mambo kufanyika kwa ufanisi zaidi. Wizara na serikali kwa
ujumla imekuwa na mahusinao mazuri na Kampuni ya Huawei Tanzania, na tumesha
shirikiana katika miradi mingi. Pamoja na ubunifu wake katika sekta ya TEHAMA,
Huawei imechangia sana katika mambo mbali mbali nchini Tanzania. Kufikia kwenye
Mkataba wa Makubaliano kati ya Wizara na Huawei ni ishara ya ubora wa kazi
ambayo kampuni hii, na itaendeleza ubadilishinaji wa teknolojia kati ya Huawei
na Tanzania. Huawei imechangia pakubwa katika ukuaji wa sekta ya TEHAMA nchini
Tanzania.
Naye Balozi
wa China nchini Tanzania Bw. Lv Youquin alisema, “ Kwa mda mrefu Tanzania na China
wamekua na mahusiano mazuri hususan baada ya ujio wa raisi wa china bwa. Xi Jinping
mwaka 2013; Kampuni nyingi za kichina zimekuja Tanzania kuwekeza na kukuza
nchi.
Kama kiongozi wa mambo ya TEHAMA duniani, Huawei imewekeza nchini
Tanzania kwa Zaidi ya miaka 17 na kwa muda wote huo imetoa ajira nyingi kwa
watanzania pamoja na kuwekeza kwenye shughuli za kijamii nchini, na
kuwa mfani wa kuiga katika maswala ya kidiplomasia kati ya Tanzania na China.
Katika
hotuba yake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof
Patrick J Makingu aliwapongeza Huawei kwa mchango wao katika kujenga Tanzania
bora kupitia TEHAMA na kuwasihi makampuni mengine ya TEHAMA kuiga mfano wa
Huawei.
Aliendelea kwa kusema, “Huawei imekuwa ikijikita katika kutafuta
suluhisho mpya katika sekta ya TEHAMA duniani. Awali mwaka huu, Huawei
ilihusika katika Kongamano la Mobile World Congress mjini Barcelona nchini
Uhispania ambapo walikuwa moja kati ya mashirika makubwa kufanya maonyesho ya
bidhaa zake mpya na sisi kama Wizara tunajivunia kufanya kazi nao”.
Naye Mtendaji Mkuu wa Huawei Tanzania Bw. Zhang Yongquan alisema “Kampuni ya Huawei Tanzania
imekuwepo nchini kwa takribani miaka 17 na imejishughulisha katika shughuli
mbalimbali za kujenga nchi ikiwepo shughuli za kijamii hususani kwenye michango
vyuoni na mahospitalini. Bw. Zhang
Yongquan, aliendelea kwa kusema “Tunashukuru serikali ya Tanzania pamoja na
wizara ya Mawasiliano,
Sayansi na Teknolojia kwa kuendelea kuiunga mkono kampuni yetu”.
Katika kongamano hilo, kampuni ya Huawei Tanzania
ilizindua bidhaa zake mpya Oceanstor V3 and Fusioncube. Pia imeonyesha Truck
yao inayozunguka nchi mbalimbali kila mara moja kwa mwaka ikianzania nchini
China, na kwa mwaka huu truck hili linazunguka kusini na magharibi mwa bara la
Afrika.
Kampuni ya Huawei Tanzania inaongoza
katika sekta ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano nchini Tanzania na imekua
ikishirikiana na wadau wengine wa mawasiliano kama Tigo, Vodacom, Airtel,
Zantel na TTCL katika kuchangia ukuaji wa watu binafsi kwenye hii sekta (ya
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano).
For
More Information please contact;
Jimmy Jinliguo, Huawei PR Manager, Cell; +255 756 516 184,
Email; jinlguo@huawei.com
About Huawei;
Huawei is a leading
global information and communications technology (ICT) solutions provider. Our
aim is to build a better
connected world, acting as a responsible corporate citizen, innovative enabler
for the information society, and collaborative contributor to the industry. Driven by customer-centric innovation and open
partnerships, Huawei has established an end-to-end ICT solutions portfolio that
gives customers competitive advantages in telecom and enterprise networks,
devices and cloud computing. Huawei’s 170,000 employees worldwide are committed
to creating maximum value for telecom operators, enterprises and consumers. Our
innovative ICT solutions, products and services are used in more than 170
countries and regions, serving over one-third of the world's population. Founded
in 1987, Huawei is a private company fully owned by its employees.
For
more information, please visit Huawei online at www.huawei.com
No comments:
Post a Comment