HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 26, 2015

SOKO LA ILALA MCHIKICHINI LAKITHIRI KWA UCHAFU,UONGOZI WALALAMA

 Mlundikano wa Takataka katika Soko la Mchikichini-Ilala jijini Dar es Salaaam ambazo zimekuwa kero kwa wafanyabiashara wa eneo hilo.
Hili ni eneo la kuegesha magari lakini wafanyabiashara wamegeuza kuwa sehemu ya kuuzia bidhaa zao  eneo katika Soko la Mchikichini-Ilala  jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Soko la Mchikichini-Ilala Jumanne Kongogo akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari waliofika katika Ofisi za Soko la Mchikichini-Ilala jijini Dar es Salaam leo,  kuhusiana na wafanyabiashara Walemavu kufunga barabara ambayo inaruhusu magari kutoka na kuingia katika soko hilo, magari ambayo yanatoa huduma katika soko hilo.
Katibu wa soko la Mchikichini-Ilala jijini Dar es Salaaam John Andrew akionyesha takataka zilivyo lundikana katika eneo la soko la Mchikichini-Ilala baada ya wafanyabiashara kuziba njia inayoruhusu magari kuingia na kutoka nje ya soko hilo, ambapo hata magari yanayochukua uchafu katika soko hilo yanashindwa kufika.kuchukua uchafu huo.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii

1 comment:

  1. Yaani sisi watu weusi, tumefeli kila nyanjaa, yaani mpaka usafi unatushinda, na mahospital duni, dawa hakuna, na hata usafi ziro, hmmmm alafu tunasema tuna Serikali, serikali upupu, Africa kuendelea ni ndoto ikiwa hata mabo madogo madogo tu kama haya ya usafi yanatushinda, tatizo , elimu duni, uaminifu ziro, uongo mwingi, kushinda ukweli

    ReplyDelete

Post Bottom Ad