Afisa mkuu Udhibiti Viatarishi Vya Malengo kutoka makao makuu NHIF Thadeus Machume(Mwezeshaji) akitoa mada kuhusu Uhamasishaji
juu ya Utaratibu wa Utoaji Mikopo ya Vifaa Tiba,Ukarabati wa Majengo na
Dawa kwa Vituo vya Kutolea Huduma za Matibabu.Alisema NHIF ikiwa na
azma ya msingi ya kuboresha huduma za matibabu kwa wanachama wake na
watanzania kwa ujumla inatoa mikopo ya vifaa tiba na ukarabati majengo
ili kusaidia watoa huduma waliosajiliwa na mfuko waweze kukarabati na
kuboresha majengo ya kutolea matibabu na kununua vifaa vya msingi.
Afisa
mkuu Udhibiti Viatarishi Vya Malengo kutoka makao makuu NHIF Thadeus
Machume alisema mikopo inayotolewa na NHIF ni mikopo ya vifaa
tiba,mikopo ya ukarabati wa vituo, na mikopo ya dawa na vitendanishi na
ili kupata mkopo unachotakiwa ni kufuata taratibu za uombaji mikopo na
sio vinginevyo.
Mgeni rasmi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga akifungua semina hiyo ambapo alisema katika mwaka wa fedha 2014/2015 NHIF mbali na kuendelea na utoaji mikopo ya vifaa tiba na ukarabati majengo,pia umeanzisha mpango mpya wa utoaji mikopo ya dawa na vitendanishi kwa vituo vyote vya kutolea huduma za matibabu vilivyosajiliwa na mfuko ikiwa ni hatua moja wapo ya kutatua tatizo la upatikanaji wa dawa na vitendanishi katika vituo vya kutolea huduma za matibabu
Mfuko
wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) leo umetoa semina kwa wadau wa afya
mkoani Shinyanga kuhusu Uhamasishaji juu ya Utaratibu wa Utoaji Mikopo
ya Vifaa Tiba,Ukarabati wa Majengo na Dawa kwa Vituo vya Kutolea Huduma
za Matibabu.Semina hiyo ya siku moja imefanyika katika ukumbi wa ofisi
ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga huku wawezeshaji wakiwa ni Dkt. Gustav
Kisamo ambaye ni afisa mdhibiti Ubora wa Afya kutoka ofisi ya Bima ya
Taifa ya Afya mkoa wa Shinyanga(kushoto) na Afisa mkuu Udhibiti
Viatarishi Vya Malengo kutoka makao makuu NHIF Thadeus
Machume(kulia)-Picha zote na Kadama Malunde-Shinyanga
Afisa mkuu Udhibiti Viatarishi Vya Malengo kutoka makao makuu NHIF Thadeus Machume akitoa mada.Aliwahamasisha wadau wa afya kufika katika ofisi za NHIF kuomba mkopo kwani ni watu wachache sana wanajitokeza kuchukua mikopo hali inayofanya pesa iendelee kubaki NHIF kutokana na kukosa watumiaji huku vituo vya afya vikiendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa dawa.
Wadau wa afya wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini |
Dkt Daniel Maguja kaimu mganga mkuu mkoa wa Shinyanga akichangia mawili matatu katika semina hiyo |
Afisa mkuu Udhibiti Viatarishi Vya Malengo kutoka makao makuu NHIF Thadeus Machume akisisitiza jambo katika semina hiyo |
Maafisa kutoka NHIF wakifurahia jambo wakati Mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam akizungumza |
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini |
******************
Imeelezwa kuwa bado
kuna mwitikio mdogo wa vituo vya afya nchini kuchukua mikopo ya vifaa
tiba,ukarabati wa vituo,dawa na vitendanishi kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF).
Hayo yamesemwa leo na
Afisa
mkuu Udhibiti Viatarishi Vya Malengo kutoka makao makuu NHIF Thadeus Machume wakati wa kikao juu ya Uhamasishaji
juu ya Utaratibu wa Utoaji Mikopo ya Vifaa Tiba,Ukarabati wa Majengo na Dawa
kwa Vituo vya Kutolea Huduma za Matibabu kilichofanyika katika ukumbi wa mkuu
wa mkoa wa Shinyanga.
Alisema bado mwitikio ni
mdogo wa kuchukua mkopo wadau wanaotoa huduma kupitia mfuko huo jambo
ambalo ni changamoto ambayo wanaendelea kuifanyia kazi.
Alisema kuanzishwa
kwa mikopo ya vifaa tiba mwaka 2008 mpaka Desemba 2014 kiasi cha shilingi
10.24 bilioni kiliidhinishwa kwa ajili ya vituo 194 vilivyoomba ni 146
vilikidhi masharti na kuchukua mkopo wa jumla ya shilingi 5.344 bilioni.
Aidha alisema kwa
upande wa mikopo ya ukarabati wa vituo vya kutolea huduma mikopo kiasi cha
shilingi 6.8 bilioni kiliidhinishwa na iliyokidhi masharti na kuchukuliwa ni
shilingi 2.14 bilioni hivyo kuwataka wadau wa afya kujitokeza kuchukua mikopo
kwani pesa ipo ya kutosha kwa ajili ya kunusuru vituo vya afya nchini.
“Vituo vingi vya afya
vina changamoto ya uhaba wa dawa,vifaa tiba na uchakavu wa majengo,lakini watu
wachache sana wanajitokeza kuchukua mikopo,tunaomba sasa mfike kwenye ofisi za
bima kwani hakuna mashari magumu wala hauhitaji kutoa rushwa ili kupata
mkopo”,alisema Machume.
Naye afisa
mdhibiti Ubora wa Afya kutoka ofisi ya Bima ya Taifa ya Afya mkoa wa Shinyanga Dkt. Gustav Kisamo ,
aliwashauri wadau hao kutumia mikopo ya vifaa tiba,madawa na vitendanishi
sanjari na ukarabati wa majengo ili kuondoa changamoto zilizopo na kuboresha
huduma kwa wagonjwa .
“Pesa huwa tunaweka
kwenye akaunti za wa kurugenzi wa halamshauri za wilaya lakini tunashauri kila
kituo cha afya kiwe na akaunti yake,vituo vya afya vinapaswa kubadilika sasa
ili kuwa msaada mkubwa zaidi kwa wananchi”,aliongeza Dkt. Kisamo.
Kwa upande wake afisa utumishi mkoa wa
Shinyanga Raymond Kiwesa alisema kutokana na kuwepo kwa changamoto ya
upatikanaji wa madawa hivyo mikopo inayotolewa na NHIF itakuwa ni fursa nzuri
kwa maslahi ya wananchi.
Katika hatua nyingine
alivitaka vituo vya huduma za afya
kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na watumishi wake kutoa kauli nzuri
kwa wateja wao ,hatua ambayo itasaidia kuongeza idadi ya wanachama wa mfuko wa
bima ya afya ya Taifa NHIF sanjari na kuboresha upatikanaji wa madawa na
vifaa tiba.
Kwa upande wake kaimu
mganga mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Daniel Maguja alionyesha wasiwasi
juu ya mikopo inayotolewa kwa kile alichodai kutokuwa na uwazi, huku akiutaka
mfuko wa taifa wa bima ya afya kurekebisha mapungufu yaliyopo ili kuongeza
idadi ya vituo vitakavyochukua mikopo.
Na Kadama
Malunde-Shinyanga
No comments:
Post a Comment