HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, May 12, 2015

NEC KUTANGAZA MAJIMBO MAPYA YA UCHAGUZI MKUU 2015, JUNI 31

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.

MAJIMBO mapya ya uchaguzi kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) mwishoni mwa Juni, ili kuweza majimbo hayo kupata wabunge watakaowakilisha wananchi hao.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,Kaimu Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ,Kailima Ramadhani amesema ugawaji huo utakuwa umezingatia idadi ya watu,jiografia ya eneo husika pamoja mawasiliano na uchumi ili kuweza kuwalishwa na bunge katika maendeleo ya jimbo.

Ramadhan amesema katika Wilaya mpya zote zinaingia katika jimbo la uchaguzi kinachobaki ni kupata maombi ya majimbo mengine kutoka kwa Makatibu Tawala wa Mikoa (RAC).

Amesema kuwa baada ya maombi hayo tume ya Uchaguzi ya Taifa itapitia mipaka pamoja na kugawa kata kutokana na kata moha haiwezi ikawa katika majimbo mawili.

“Tunachotaka ni makatibu Tawala wa Mikoa kuleta maombi yao mapema na kuweza kuyapitia na katika mipaka pamoja na vigezo vilivyoanishwa na NEC”amesema Ramadhan.
 Kaimu Mkurugenzi Tume ya Taifa ya Uchaguzi Kailima Ramadhan akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC), juu ya ugawaji wa majimbo mapya ya uchaguzi jijini Dar es Salaam leo.
 Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa NEC akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari hawapo pichani walipokutana leo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya  wanahabari wakifuatilia katika mkutano wa NEC uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.(PICHA NA EMMANUEL MASSAKA,GLOBU YA JAMII)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad