Sehemu wa Wajumbe kutoka nchi 47 zinazounda Kamisheni ya Idadi ya Watu na Maendeleo. wajumbe wa kamisheni hii, 12 wanatoka nchi za Bara la Afrika , 11 kutoka Bara la Asia na Pacific, 5 kutoka nchi za Ulaya Mashariki, 9 wanatoka Latini ya Amerika na Visiwa na Karibiani, na 10 wanatoka Nchi za Ulaya Magharibi na Mataifa mengine. Wajumbe hawa huchaguliwa na Baraza Kuu la Uchumi la Umoja wa Mataifa ( ECOSOC).
Naibu
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi
Ramadhan Mwinyi akizungumza wakati wa Mkutano wa 48 wa Kamisheni ya
Idadi ya Watu na Maendeleo, Tanzania ni mjumbe wa Kamisheni hii ikiwa
ni kati ya nchi 12 kitoka Afrika zikiliwakilisha Bara ya Afrika.
pamoja na naye ni Bw. Seif Shaban Mwinyi, Kamishna wa Mipango kutoka
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Bw. Stephen Kiberiti kutoka Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii.
Bi. Samira Diria, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa KImataifa, na Bi. Esther Suvi kutoka Kamisheni ya Mipango, ambao ni sehemu ya Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 48 wa Kamisheni kuhusu Idadi ya watu na maendeleo wakifuatilia majadiliano ya jumla.
No comments:
Post a Comment