HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 6, 2015

WAZIRI MKUU AWAPA POLE WAFIWA, MAJERUHI KAHAMA

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa pole wanafamilia wa MzeeZakaria  Limbe ambao wamepoteza wototo wane katika mafa ya mvua kubwa yenye upepo na  mawe iliyonyesha katika eneo la Mwakata Machi  3 usiku. Alikwenda katika maeneo yaliyoathirika leo  kuwapa pole wananchi. 
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipa pole Shoma Petro  ambaye ni mmoja wa majeruhi wa maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa yenye upepo na mawe iliyonyesha kwenye  eneo la  Mwakata wilayani Kahama Machi 3, 2015 usiku. Mheshimiwa Pinda alikwenda kwenye hospitali a wilaya ya Kahama kuwapa pole  majeruhi waliolazwa hospitalini hapo.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimpa pole Mzee  Donald Lubunda ambaye  amepoteza watoto wane katika maafa yaliyosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha  katika  eneo la Mwakata wilayani Kahama Machi 3 usiku. Mheshimiwa Pinda alikwenda kuwapa pole waathirka leo

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Waziri wa Nchi Ofisi yaWaziri Mkuu, Jenista Mhagama  (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa ShinyangaDr Rufunga kukagua maeneo yalyoathiriwa na mvua kubwa iliyoambatana  na upepo mkali na mawe katika eneo  Mwakata wilayani Kahama usiku Machi 3, 2015. Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ametembelea baadhi ya familia zilizopoteza wapendwa wao pamoja na majeruhi waliolazwa kwenye hospitali ya wilaya ya Kahama kutokana na maafa ya mvua ya mawe iliyonyesha usiku wa kuamkia jana.

Akizungumza na wafiwa katika vijiji vya Mwakata na Magugung’hwa katika kata ya Mwakata wilayani Kahama leo mchana (Alhamisi, Machi 5, 2015) Waziri Mkuu alisema Serikali haitawaacha katika kipindi hiki kigumu walichonacho.

Waziri Mkuu pia alitumia fursa hiyo kuwafikishia wafiwa na waathirika wa maaafa hayo salamu kutoka kwa Rais Jakaya Kikwete ambaye aliwaomba wawe na subira katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.

Akiwa katika shule ya msingi Mwakata ambako watu 250 wanahifadhiwa hapo kwa muda, Waziri Mkuu aliwaambia wakazi hao pamoja na wananchi waliofika kumsikiliza kwamba Serikali imepanga kuleta vyakula, mahema, mablanketi na madawa ya hospitali ili kuwasaidia waathirika hao. “Serikali haitaacha mtu afe kwa njaa,” alisema.


Pia aliagiza maghala ya NFRA yaliyoko Isaka yatumike kupokea misaada ya chakula kwa sababu yako karibu sana kata ya Mwakata. “Ili uratibu wa misaada uweze kufanyika hapa kijijini, ni vema maghala ya kuhifadhi chakula cha msaada yakahamia hapa Isaka kwa sababu ni karibu sana na hapa Mwakata,” alisema.

“Yakiwa hapa itasaidia usimamizi na uhakika wa huduma zinazotolewa kwa waathirika. Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya simamieni hilo kwa sababu janga hili ni letu na linabebwa na Serikali,” aliongeza.

Alisema ameongea na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid na kumwagiza atume watu wake wafanye tathmini ya hali ya afya kwani katika hali ya majanaga kama haya, ni lazima kuna hatari ya kutokea kwa magonjwa ya mlipuko.

Mapema, Mbunge wa Msalala, Bw. Ezekiel Maige aliiomba Serikali itume misaada ya haraka ya vyakula na mahema kwa waathirika hao lakini pia ipeleke kikosi cha wanajeshi ili wasaidie kujenga nyumba za watu walioathirka kama ambavyo ilifanya kwa watu wa Kilosa mwaka 2009.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), Bibi Jenista Mhagama ambaye anasimamia idara ya maafa ameuagiza uongozi wa wilaya ya Kahama kuhamishia timu ya waratibu wake kwenye eneo la tukio badala ya kufanyia kazi kutoka makao makuu ya wilaya ambako ni zaidi ya km. 30.

“Misaada iasche kuratibiwa wilayani bali ihamie hapa Mwakata, na hao wanaotoa misaada waambiwe wailete hapa kwenye eneo la tukio … uratibu ukifanyika kule hakuna atakayekuwa na picha halisi ya nini kinaendelea kwenye kijiji hiki,” alisisitiza.

Mvua hiyo imesababisha vifo vya watu 42 na kujeruhi watu 98 huku mamia watu wakiwa hawana mahali pa kuishi. Pia watu 52 kati ya 112 waliokuwa wamelazwa hospitalini wameruhusiwa kurudi majumbani huku majeruhi 60 wakiendelea kupatiwa matibabu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad