Shirika lisilo la kiserikali la Brien Holden Vision Institute kupitia mradi wa Afya ya Macho Mashuleni (Seeing is Believing) unaofadhiliwa na benki ya Standard Chartered limekabidhi msaada wa vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 48, kwa hospitali za wilaya za Mbozi,Ileje na Kyela zote za mkoa wa Mbeya ambapo msaada huo utawanafaisha wanafunzi kwa kupata huduma ya kupima na kutibiwa bure.
Mratibu wa Taifa wa Huduma za Macho, Dkt.Nkundwe Mwakyusa (katikati) akisistiza jambo wakati alipokuwa akiongea na wataalamu wa macho kutoka katika wilaya za Kyela ,Ileje,na Mbozi (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 48, vilivyotolewa na Shirika lisilo la kiserikali la Brien Holden Vision Institute kupitia mradi wa Afya ya Macho Mashuleni (Seeing is Believing) unaofadhiliwa na benki ya Standard Chartered kwenye hospitali za wilaya hizo za mkoa wa Mbeya. Kulia ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa, Constantine Mushi na Mratibu wa mradi huo Violeth Shirima.
Mratibu wa Huduma za Macho mkoa wa Mbeya, Dkt.Faraji Killewa (kulia) akisoma takwimu za magonjwa ya macho kwa watoto wa mkoa huo, wakati wa hafla ya kukabidhiwa vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 48, kwa ajili ya hospitali za wilaya za Ileje,Mbozi, na Kyela iliyofanyika katika hospitali hiyo. Wa pili kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Seif Mhina, Kaimu Katibu Tawala Mkoa Constantine Mushi, Mratibu wa Taifa wa Huduma za Macho Dkt.Nkundwe Mwakyusa na Mratibu wa mradi huo Violeth Shirima. Mradi huo umefadhiliwa na benki ya standard Chartered kwa mikoa ya Mbeya na Mwanza.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa Constantine Mushi, akimkabidhi Kaimu Mkurugenzi Wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya, Elisey Nngoi mashine ya komputa ya kupima macho, wakati wa hafla ya kukabidhiwa vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi 48 kwa ajili ya Hospitali za wilaya za Ileje, Mbozi, na Kyela. Mradi huo umefadhiliwa na Benki ya Standard Chartered kupitia shirika lisilo la kiserikali la Brien Holden Vision Institute kwa ajili ya kutoa huduma za macho kwa watoto wa shule za msingi,huduma hiyo itawawezesha watoto hao kupata matibabu bure ya macho pindi wanapogundulika. Kulia ni mratibu wa maradi huo Violeth Shirima.
Mratibu wa Mradi wa Huduma za Macho Shule za Msingi unaofadhiliwa na benki ya Standard Chartered (Seeing is Believing) kutoka shirika lisilo la kiserikali la Brien Holden Vision Instutite, Violeth Shirima (kulia) akimkabidhi msaada wa vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 48 Muuguzi Msaidizi wa Huduma za Macho wa Hospitali ya Wilaya ya Kyela, Monica Francis (wa tatu toka kushoto) wakati wa hafla iliyofanyika katika hospitali ya mkoa wa Mbeya. Wanafunzi wa shule za msingi za halmashauri za Mbozi, Ileje na Kyela watanufaika na msaada huo wa kutibiwa magonjwa ya macho bure.
Mratibu wa Mradi wa Huduma za Macho Shule za Msingi unaofadhiliwa na benki ya Standard Chareterd (Seeing is Believing) kutoka shirika lisilo la kiserikali la Brien Holden Vision Institute, Violeth Shirima (kulia) akimuonyesha Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya miwani inayotengenezwa na shirika lake kwa ajili ya kuwagawia watoto mashuleni wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wavifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 48 kwa hospitali za wilaya za Mbozi, Ileje na Kyela zote za Mkoani Mbeya.
Mratibu wa Mradi wa Huduma za Macho Shule za Msingi unaofadhiliwa na benki ya Standard Chartered (Seeing is Believing) kutoka shirika lisilo la kiserikali la Brien Holden Vision Institute, Violeth Shirima (kulia) akimkabidhi msaada wa sanduku la vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 48 Muuguzi Msaidizi wa Huduma za Macho wa Hospitali ya Wilaya ya Kyela, Monica Francis (kulia) wakati wa hafla iliyofanyika katika hospitali ya mkoa wa Mbeya ambapo wanafunzi wa shule za msingi za Halmashauri za Mbozi, Ileje na Kyela watanufaika na msaada wa kupima macho na kutibiwa magonjwa ya macho bure.
Kaimu Afisa Elimu wa Wilaya ya Kyela Kassim Mtili (kulia), Mratibu wa Huduma za Afya Mashuleni wa wilaya hiyo, Leah Mwakapala (katikati) na Muuguzi Msaidizi wa Huduma za Macho wa Hospitali ya Wilaya ya Kyela, Monica Francis wakikagua mashine ya komputa ya kupima macho mara baada ya kukabidhiwa msaada wa vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 48 na Mratibu wa Mradi wa Huduma za Macho Shule za Msingi unaofadhiliwa na benki ya Standard Chareterd (Seeing is Believing) kutoka shirika lisilo la kiserikali la Brien Holden Vision Institute Violeth Shirima (kulia) wakati wa hafla iliyofanyika katika hospitali ya mkoa wa Mbeya.
Mratibu
wa Mradi wa Macho kwa shule za msingi kupitia mradi wa afya ya macho
kwa mtoto unaofadhiliwa na benki ya Standard Chartered (Seeing is
Believing) kutoka shirika lisilo la kiserikali la Brien Holden Vision
Institute Violeth Shirima (kushoto) akimkabidhi msaada wa sanduku la
vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 48 Muuguzi Msaidizi
wa Huduma za Macho wa Hospitali ya Wilaya ya Kyela, Monica Francis
(kulia) wakati wa hafla iliyofanyika katika hospitali ya mkoa wa Mbeya.
Wanafunzi wa shule za msingi za halmashauri za Mbozi, Ileje , Kyela
watanufaika na msaada huo wa kutibiwa magonjwa ya macho bure.
Wanaoshuhudia: wa pili kutoka kulia ni Kaimu Afisa Elimu wa Wilaya ya
Kyela, Kassim Mtili na Mratibu wa Huduma za Macho Mashuleni, Leah
Mwakakapala.
Kaimu
Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Constantine Mushi akikabidhiwa msaada wa
mashine ya Kompyuta inayopima macho (Autorefractor) na Mratibu wa Huduma
za Macho kwa watoto wa shule za msingi kupitia mradi wa Afya ya Macho
kwa Mtoto (Seeing is Believing) unaofadhiliwa na benki ya Standard
Chartered, Violeth Mushi , wakati wa hafla iliyofanyika katika hospitali
ya Mkoa wa Mbeya. Jumla ya vifaa vvyenye thamani ya shilingi milioni 48
vilikabidhiwa kwa hospitali za wilaya za Mbozi, Ileje na Kyela.
Kaimu
Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Constantine Mushi akikabidhiwa msaada wa
sanduku la vifaa vya macho na Mratibu wa Huduma za Macho kwa watoto wa
shule za msingi kupitia mradi wa Afya ya Macho kwa Mtoto (Seeing is
Believing) unaofadhiliwa na benki ya Standard Chartered, Violeth leth
Mushi ,wakati wa hafla iliyofanyika katika hospitali ya mkoa wa Mbeya.
Jumla ya vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 48 vilikabidhiwa kwa
hospitali za wilaya za Mbozi, Ileje na Kyela. Mradi huo utawanaufaisha
wanafunzi wa wilaya hizo kwa kupata matibabu bure pamaoja na miwani mara
baada ya kugundulika kama wanamatatizo ya macho ili weweze kusoma
vizuri.
Mratibu
wa Taifa wa Huduma za Macho, Dkt.Nkundwe Mwakyusa (kushoto)
akiwaelekeza wataalamu wa macho kutoka katika hospitali ya Wilaya ya
Kyela jinsi ya kutumia vipimo vya macho mara baada ya kukabidiwa msaada
wa vifaa hiyo vyenye thamani ya shilingi milioni 48. Kulia ni Muuguzi
Msaidizi wa hospitali hiyo Monica Francis, Kaimu Afisa Elimu Wilaya
Kassim Mtili na Mratibu wa Huduma za Macho Mashuleni wa Wilaya Leah
Mwakapala, mradi huo umefadhiliwa na benki ya Standard Chartered kwa
wilaya za mkoa wa Mbeya na Mwanza. Wa pili kutoka kushoto ni Mratibu wa
Macho Mashuleni toka shirika lisilo la kiserikali la Brien Holden Vision
Institute, Violeth Shirima.
Mwalimu
wa shule ya msingi Itete iliyopo katika kijiji cha Mlowo Wilaya ya
Mbozi, Katalina Mwilyugule akiwafundisha wanafunzi wa darasa la Nne somo
la Hesabu huku wote wakiwa wamekaa kwenye madawati, shule hii ni moja
ya shule zinazonufaika na mradi wa Afya ya Macho kwa Mtoto unaofadhiliwa
na benki ya Standard Chartered ,ambapo wanafuzi wa shule hiyo wanapata
huduma ya kupima macho na matibabu bure ili waweze kusoma vizuri.shirika
lisilo la kiserikali lilitoa msaada wa vifaa vya macho kwa watoto kwa
wilaya za Mbozi, Ileje naKyela vyenye thamani ya shilingi milioni 48.
No comments:
Post a Comment