Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam wakiendelea na ushonaji wa nguo za aina mbalimbali kama wanavyoonekana katika picha. Jeshi la Magereza nchini linatekeleza ipasavyo jukumu lake la Urekebishaji kwa kuwapatia ujuzi wa fani mbalimbali Wafungwa wanapokuwa wakitumikia vifungo vyao Magerezani.
Wafungwa
wa Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam wakikata vitambaa vya nguo
kabla ya kuanza kushona nguo za Wafungwa Magerezani. Wafungwa hao
hujifunza Stadi mbalimbali za ujuzi ambazo huwasaidia kujipatia kipato
mara tu wanapomaliza kifungo chao.
Aina za nguo mbalimbali ambazo tayari zimeshonwa kwa Ustadi Mkubwa na Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga Dar es Salaam. Gereza Kuu Ukonga Dar es Salaam limejizolea umaarufu mkubwa hapa nchini kwa kutekeleza ipasavyo Programu mbalimbali za Urekebishaji wa Wafungwa kwa Vitendo

Mkuu wa Kiwanda cha Gereza Kuu Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Ismail Mlawa akiongea na Wanahabari(hawapo pichani).Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza

No comments:
Post a Comment