HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 14, 2015

USIOMBE KUKUTANA NA HAWA JAMAA WANAOKAMATA PIKIPIKI ZINAZOINGIA KATIKATI YA MJI BILA VIBALI

 Leo nikiwa katika pita pita zangu za Mtaa kwa Mtaa,nipita eneo hili la Daraja la Salenda ambapo ni moja ya kituo cha hawa jamaa wanaokamata pikipiki zinazoingia kwenye maeneo ya katikati ya jiji la Dar es salaam bila ya kuwa na kibali maalum.sina tatizo na kukamatwa kwa pikipiki hizo,ila ni ule utaratibu wanaoutumia jamaa hawa kuzikamata pikipiki hizo.kuna wakati wanazizuia pikipiki hizo zikiwa kwenye mwendo,bila kujali usalama wa mwendeshaji,mpakiwaji na hata yeye mwenyewe mkamataji,maana wanatabia ya kukimbilia kwenye swichi na kuizima pikipiki hiyo na kuchomoa funguo,jambo ambalo si salama hata kwa pikipiki yenyewe.Jambo hili linapaswa kuangaliwa tena kwa jicho lingine,maana linaweza kuja kuleta madhara makubwa siku moja.
Pichani ni Mmoja wa wakata pikipiki hizo akiwa ameizuia pikipiki hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad