Katika adhima ya kufikisha mawasiliano vijijini, Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) imezindua mnara wa mawasiliano ya simu katika kata ya Pagwi, wilaya ya Kilindi Mkoa wa Tanga.
Akihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria tukio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Selemani Liwowa alisema kwa kupata mawasiliano itasaidia wananchi kuwasiliana pamoja na kutafuta fursa mbalimbali kwa ajili maendeleo. Aidha, Mkuu wa Wilaya alisisitiza wananchi kutumia mawasiliano ya simu kwa ajili ya shughuli za maendeleo na usalama wa mali zenu pamoja na nchi kwa ujumla.
“Nawaombeni pia tumieni fursa hii ya uwepo wa mawasiliano kwa ajili ya kukuza uchumi wa Kata hii, kutafuta masoko nje na ndani ya mkoa wa Tanga” alisema Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Selemani Liwowa.
Naye Meneja wa TTCL mkoa wa Tanga alisema kuwa mnara huo unatoa huduma ya mawasiliano katika vijiji vya Lumotio, Pagwi, Makelele, Masilei, Kwekivu na maeneo yote yanayozunguka vijiji hivyo.
Lusama alifafanua kuwa kupitia mfuko unaosimamia utoaji wa huduma ya Mawasiliano kwa wote nchini (UCSAF), TTCL ilipewa jukumu la kufikisha huduma za mawasiliano katika kata 20 kwa awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi wa mawasiliano vijijini. Katika Kata hizo za mwanzo Pagwi ni moja ya Kata zilizonufaika na mradi huo.
Meneja wa Mkoa wa Tanga wa TTCL, Peter Lusama akitoa hotuba siku ya Uzinduzi wa Mnara wa Mawasiliano katika kata ya Pagwi, Wilaya ya Kilindi, Tanga.
Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Selemani Liwowa akizungumza na wananchi waliohudhuria kwenye uzinduzi wa Mnara wa Mawasiliano wa Pagwi, Wilaya ya Kilindi, Mkoani Tanga. Mnara huu umesaidia wananchi wa maeneo hayo kupata mawasiliano ya simu.
Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Selemani Liwowa akikata utepe, kuashiria uzinduzi rasmi wa mnara wa mawasiliano wa Pagwi, Wilaya ya Kilindi, Tanga.
Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Selemani Liwowa na baadhi ya wageni walikwa wakikagua eneo ambalo limejengwa mnara wa mawasiliano ya Simu wilayani Kilindi mkoani Tanga.
Kikundi cha burudani kikitumbuiza siku ya uzinduzi wa Mnara wa Mawasiliano ya Simu wa TTCL, hafla hii ya uzinduzi ulifanyika katika kata ya Pagwi, wilayani Kilindi, Mkoani Tanga.
Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Selemani Liwowa akipokea zawadi ya modem kutoka kwa Meneja wa Mkoa wa Tanga wa TTCL, Peter Lusama
Mgeni Rasmi, Mkuu wa Wilaya ya Kilindi Selemani Liwowa akipokea zawadi ya Simu ya mezani kutoka kwa Meneja wa Mkoa wa Tanga wa TTCL, Peter Lusama

No comments:
Post a Comment