HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 1, 2015

TANGAZO LA KUZIMWA KWA MTAMBO WA MAJI RUVU CHINI KUTOKANA NA MATENGENEZO YA BOMBA KUBWA


SHIRIKA LA MAJI SAFI NA MAJITAKA DAR-ES-SALAAM (DAWASCO),
LINAWATANGAZIA  WAKAZI WA JIJI LA DAR-ES-SALAAM NA MJI WA BAGAMOYO MKOANI PWANI  KUWA, MTAMBO WA KUZALISHA MAJI WA RUVU CHINI UMEZIMWA KWA SAA 24 KUANZIA ASUBUHI YA TAREHE 01.03.2015. 

KUZIMWA KWA MTAMBO WA RUVU CHINI KUMETOKANA NA MATENGENEZO YA BOMBA LA INCH 54 ENEO LA MATANKI YA CHUO KIKUU.

MATENGENEZO YANAENDELEA NA YANATARAJIA KUKAMILIKA BAADA YA SAA 24.

 KWASABABU HIYO MAENEO YAFUATAYO YATAKOSA MAJI:
MJI WA BAGAMOYO, VIJIJI VYA MAPINGA, KEREGE NA MAPUNGA. BUNJU, BOKO, TEGETA, KUNDUCHI, SALASALA, JANGWANI, MBEZI BEACH NA KAWE.
MAENEO MENGINE NI MLALAKUWA, MWENGE, MIKOCHENI, MSASANI, SINZA, MANZESE, MABIBO, KIJITONYAMA, KINONDONI, OYSTERBAY, MAGOMENI, UPANGA, KARIAKOO, CITY CENTRE, ILALA, UBUNGO MAZIWA, KIGOGO, MBURAHATI, HOSPITALI YA RUFAA MUHIMBILI, BUGURUNI, CHANGOMBE NA KEKO.       
         
WANANCHI MNASHAURIWA KUHIFADHI MAJI NA KUYATUMIA KWA MATUMIZI YA LAZIMA.

DAWASCO INAWAOMBA RADHI KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA
KWA MAWASILIANO ZAIDI PIGA SIMU HUDUMA KWA WATEJA 022 5500240-4 NA 0658-198889

IMETOLEWA NA OFISI YA UHUSIANO
DAWASCO-MAKAO MAKUU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad