Afisa
Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (kulia), akipena mikono na
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Vingunguti-Butiama jijini Dar es Salaam,
Elvis Bwahama, wakati akikabidhi msaada wa mifuko ya saruji tani 3 na mabati,
kwa ajili ya ujenzi kwenye kituo cha kulea watoto walio katika mazingira
magumu, cha Lukema. Hafla ya kukabidhin msaada huo kwa kituo hichomnkinacholea
watoto 70, ilifanyika Ijumaa Machi 6, 2015. Kushoto ni mwenyekiti wa kituo
hicho, Fatuma Ramadhani.
Afisa
Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (kulia), akiteta jambo na
mmoja wa watoto wanaolelewa kwenye kituo cha kulea watoto walio katika
mazingira magumu cha Lukema, kilichoko Vingunguti-Butiama jijini Dar es Salaam
Ijumaa Machi 6, 2015. Mfuko huo umetoa msaada wa saruji na mabati kwa ajili ya
kupanua ujenzi wa kituo hicho kinacholea watoto 70 kwa sasa
Afisa
Uhusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (kulia), akizungumza jambo wakati alipofika kutoa msada wa saruji na mabati kwa niaba ya Mfuko huo kwa kituo cha kulea watoto waishio katika mazingira magumu, kituo cha Lukema, Vingunguti-Butiama jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Machi 6, 2015.
Mwenyekiti
wa Kituo cha kulea watoto walio katika mazingira magumu cha Lukema, kilichoko
Vingunguti-Butiama jijini Dar es Salaam, Fatuma Ramadhani, akizungumza kwenye
hafla ya kupokea msaada wa saruji na mabati vilivyotolewa na Mfuko huo kwa
ajili ya ujenzi.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa
Vingunguti-Butiama jijini Dar es Salaam, Elvis Bwahame, (kushoto), akizungumza
wakati wa hafla hiyo ya makabidhiano. Kulia ni mkurugenzi wa kituo, Lukondo
Mchundo
No comments:
Post a Comment