Dr. Natalius Kapilima wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya akimpima shinikizo la damu
Bw. Exadius Nthono wa Lesotho katika mkutano wa mwaka wa wahasibu waandamizi
unaofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere ambapo NHIF inatoa
huduma za upimaji afya bure.
Na Catherine Kameka
WADAU wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wameuomba Mfuko huo
kuendeleza programu za upimaji wa afya bure ili kuwasaidia wanachama
wake na wananchi kwa ujumla kujua hali za afya zao lakini pia kuepekana
na maradhi yasiyoambukiza.
Hayo wameyasema Dar es Salaam jana katika mkutano wa Wahasibu
Waandamizi wa nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika, unaofanyika
katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu J.K.Nyerere ambapo NHIF ilishiriki
kwa kuwa na banda la elimu kwa umma na upimaji wa afya bure
uliokwenda sambamba na utoaji wa elimu ya namna ya kujikinga na
maradhi yasiyoambukiza kama moyo na mengine.
Pamoja na ombi hilo, NHIF imekuwa ikiendesha upimaji katika maeneo
mbalimbali ya nchi kwa lengo la kuwasaidia wananchi kufahamu afya zao
lakini pia kuwapa ushauri wa namna ya kujikinga na maradhi hayo ambayo
yamekuwa yakiongezeka kwa kasi na matibabu yake ni ya ghari.

Katika dawati la elimu kwa umma ililitolewa elimu ya umuhimu wa kujiunga
na NHIF, haki na wajibu kwa mwanachama wa NHIF wakati wa kupata
huduma.
Wakizungumza katika banda la Mfuko washiriki wa mkutano huo walisema
huduma zinazotolewa na Mfuko ni nzuri na ni za kuigwa kwa kuwa
zimelenga kuelimisha jamii umuhimu wa kupima afya kabla ya kuugua
hasa katika kipindi hiki ambapo gharama za matibabu zimekuwa ni kubwa.
Akitoa ushauri wa jumla kwa washiriki hao, Ofisa Udhibiti Ubora wa NHIF,
Dk. Raphael Mallaba, alisema kuwa ni vyema wakawa na utamaduni wa
kupima afya zao mara kwa mara hali itakayowasaidia kujitambua kutokana
na ukweli kwamba magonjwa haya kwa sasa yanaongezeka na matibabu
yake ni ya ghari.
Alisema kuwa magonjwa haya yanasababishwa na hali halisi ya maisha
iliyopo sasa hivyo ni vyema mkakati wa kufuatilia afya ukawa kwa kila mtu
kwa kuwa bila kuwa na afya njema hata maendeleo ya jamii zetu
zitayumba.
No comments:
Post a Comment